Swali 8: Je, msemo huu ni sahihi:

“Kutukana Allaah na kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si ukafiri kwa dhati yake, bali ni ishara na alama ya dharau na kuidunisha dini iliyomo moyoni.”?

Jibu: Maneno haya si sahihi, bali ni ´Aqiydah ya Murji-ah na ni ´Aqiydah batili. Bali tusi lenyewe ni ukafiri na mzaha wenyewe ni ukafiri. Amesema (Ta´ala):

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”  Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]

Allaah amewahukumu ukafiri baada ya imani kwa sababu ya maneno yao. Hajasema ikiwa mlikuwa mnaamini moyoni mwenu chochote. Alllaah (Ta´ala) amewaita kuwa ni makafiri kwa maneno yao haya. Kwa hiyo ikajulisha ya kwamba maneno au neno la kufuru si ukafiri na kwamba eti ni alama ya kilichomo moyoni ni batili. Hakuna anayejua yaliyomo ndani ya moyo isipokuwa Allaah (Ta´ala). Ukafiri unakuwa kwa moyo, kwa maneno na kwa matendo. Kwa kifupi ni kwamba maneno hayo juu yanaenda sambamba na madhehebu ya Murji-ah.

[1] 09: 65-66

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 25
  • Imechapishwa: 05/01/2026