8 – Abu Thaabit ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Haazim ametuhadithia, kutoka kwa al-´Alâ’ bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
من صلَّى عليَّ صلى الله عليه عشراً
”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]
[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Wanamme wake ni wanamme Swahiyh. Abu Thaabit anaitwa Muhammad bin ´Ubaydillaah bin Muhammad al-Madaniy. Kisha imesimuliwa kupitia njia nyingine kutoka kwa al-´Alaa na njia nyingine ya tatu (11).
- Muhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 28
- Imechapishwa: 15/03/2023
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy