08. Dalili ya sita kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

6- Abu Muhammad ´Abdullaah bin Mansuur bin Hibatillah bin al-Mawsiliy ametuhadithia: Abul-Husayn al-Mubaarak bin ´Abdil-Jabbaar as-Sayrafiy ametuhadithia: Abul-Hasan Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin Ja´far ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym bin al-Hasan bin Shaadhaan ametuhadithia: Abu ´Abdillaah Ahmad bin Muhammad bin al-Mughallas ametuhadithia: Abu ´Uthmaan Sa´iyd bin Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Ibn Ishaaq amesema:

“Kuna mtumwa mweusi ambaye alikuwa akimilikiwa na mmoja katika watu wa Khaybar alitoka nje na kondoo wakati alipofikiwa na khabari kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefika. Akasema kuwaambia baadhi ya marafiki zake: “Mtu huyu ni nani?”Wakasema: “Ni Mtume wa Allaah aliyetumwa na Allaah.” Akasema: “Yule aliye mbinguni?”Wakajibu: “Ndio.”Akasema: “Niacheni niwe karibu naye.”Walipompeleka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Je, wewe ni Mtume wa Allaah?” Akajibau: “Ndio.”Akauliza: “Yule aliye mbinguni?” Akajibu: “Ndio.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  akamuamrisha atamke shahaadah ambapo akatamka. Akawaelekea kondoo wake, akawatupia nyusoni mwao changarawe kisha akasema: “Nenda zako! Ninaapa kwa Allaah sintokuandama tena kamwe.”Akaenda zake na hayo ndio ya mwisho aliyoyaona. Mtumwa yule akapigana mpaka akafa akiwa ni shahidi kabla ya kuwahi kuswali swalah hata moja. Mwili wake ukapelekwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo ukawekwa nyuma yake. Akamwelekea kisha akampa mgongo tena. Kukasemwa: “Ee Mtume wa Allaah! Ulimwelekea kisha ukampa mgongo tena?”Akasema: “Hivi sasa yuko na mke wake katika wanawake wa Peponi. Mtumwa huyo alikuwa akiitwa Aslam.”[1]

Ameipokea al-Umawiy katika “al-Maghaaziy.”

[1] Hadiyth hii imepokelewa na al-Haakim kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesema:

”Mlolongo wa wapokezi wa Hadiyth ni Swahiyh na si al-Bukhaariy wala Muslim hawakuipokea.”

adh-Dhahabiy amesema:

”Sharahbiyl [aliyepokea kutoka kwa Jaabir] ametuhumiwa.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 22/04/2018