Amri ya kwanza iliyotajwa katika Qur-aan ni maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِbنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kucha. Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi, msimfanyie Allaah washirika hali ya kuwa nyinyi mnajua [kwamba hana washirika].”[1]

Mara nyingi tunaona katika Qur-aan tukufu ulinganizi katika Tawhiyd-ul-´Ibaadah, ikiamrishwa na majibu juu ya shubuha zinazoelekezwa kwayo. Kila Suurah katika Qur-aan, bali kila Aayah katika Qur-aan, ni yenye kulingania katika Tawhiyd hii. Kwa sababu Qur-aan ima ni maelezo kuhusu Allaah, majina, sifa na matendo Yake, hiyo ni Tahwiyd-ur-Rubuubiyyah; ulinganizi juu ya kumuabudu Yeye mmoja pekee, hali ya kuwa hana mshirika na kuacha kuabudu badala Yake, hiyo ni Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah; maelezo juu ya namna ambavyo wapwekeshaji watavyokirimiwa na kutiiwa Kwake duniani na Aakhirah, hayo ndio malipo ya Tawhiyd; maelezo kuhusu washirikina na malipo yao duniani na Aakhirah, hayo ni malipo ya mwenye kutoka nje ya hukumu ya Tawhiyd au vilevile ni hukumu na Shari´ah mbalimbali, jambo ambalo ni miongoni mwa haki za Tawhiyd. Kwani uwekaji wa Shari´ah ni haki ya Allaah pekee.

[1] 02:21-22

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 25/03/2019