41 – Muhammad bin ´Aliy bin al-Hasan ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Ash´ath ametuhadithi: Shaykh mmoja kutoka Nakh´ amenihadithia, kutoka kwa Mashaykh wake katika maswahiba wa ´Abdullaah bin Mas´uud:
“Yatosha kama ushahidi juu ya majaribio ya dini ya mtu ni kule kuwa na marafiki wengi.”
42 – Salamah amenihadithia: Sahl bin ´Aaswim ametuhadithia: Qabiyswah ametuhadithia: Nimemsikia Sufyaan akisema:
”Kuwa na ndugu wengi kunaonyesha upumbavu wa dini.”
43 – Salamah amenihadithia: Sahl amenihadithia: Nimemsikia Saalim bin Maymuun: Nimemsikia ´Uthmaan bin Zaa-idah akisema:
”Ilikuwa inasemwa kwamba ukimwona mtu ana marafiki wengi, basi tambua ya kwamba ni mtu wa kuchanganya mambo.”
44 – Kwa njia hiyohiyo amenihadithia ´Aliy bin Ma´bad: Fadhwaalah bin Swayfiy ametuhadithia:
”Abaan bin ´Uthmaan aliandika kwenda kwa mmoja katika ndugu zake: “Kama unataka dini yako kusalimika, basi punguza kutambulika.”
45 – ´Abdullaah bin Ahmad al-Khuzaa´iy amenihadithia: Nimemsikia baba yangu: Nimemsikia al-Hasan bin Rashiyd: Nimemsikia ath-Thawriy akisema:
”Ee Hasan! Usijitambulishe kwa yule asiyekujua, na kataa maarifa ya anayekujua.”
46 – Muhammad bin ´Abdil-Majiyd at-Tamiymiy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, ambaye amesema:
”Pindi watu wengi walipokuwa wanakuja katika darsa za Khaalid bin Ma´daan, basi huondoka kwa kuchelea asije kushuhurika.”
47 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Layth, ambaye amesema:
”Alikuwa pindi watu zaidi ya watatu wanapokuja kukaa kwa Abul-´Aaliyah, basi husimama akaondoka.”
48 – Haashim bin al-Waliyd ametuhadithia: Abu Bakr bin ´Ayyaash ametuhadithia:
”Nilimuuliza al-A´mash: “Uliwahi kuona watu wangapi zaidi waliokuwepo kwa Ibraahiym?” Akasema: “Wanne au watano.”
49 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Abu Bakr:
“Sikuwahi kuona kwa Habiyb bin Abiy Thaabit vijana zaidi ya watatu kamwe.”
50 – ´Aliy bin al-Ja´d ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa ´Awf, kutoka kwa Abu Rajaa’, aliyesema:
”Twalhah aliwaona watu waliokuwa wanatembea pamoja naye zaidi ya kumi, akasema: “Hawa ni nzi wa tamaa na vipepeo wa moto.”
51 – Ibraahiym bin Ziyaad Sablaan na Abu Muslim wametuhadithia: ´Abdullaah bin Idriys ametuhadithia, kutoka kwa Haaruun bin ´Antarah, kutoka kwa Sulaym bin Handhwalah, ambaye amesema:
”Tulipokuwa pamoja na Ubayy bin Ka´b tukitembea nyuma yake akamuona ´Umar, akampiga kwa mjeledi. Akasema: ”Angalia, ee Kiongozi wa waumini kile unachokifanya.” Akasema: “Hakika hii ni utwevu kwa anayefuata na ni fitina kwa anayefuatwa.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 68-77
- Imechapishwa: 22/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 68-77
Imechapishwa: 22/01/2026
https://firqatunnajia.com/07-walikuwa-wakikimbia-wasitambulike/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket