07. Usipochagua njia sahihi, hatimae utajichosha

Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba kuna njia za kujifunza elimu. Tunaona baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa wamejichosha miili yao na nafsi zao, lakini hawaoni kuwa wanapata elimu yoyote. Wanasema kuwa wamefuatilia mizunguko ya kielimu miaka na miaka, kusoma vitabu na kutembea navyo huku na kule, lakini hawakufikia elimu yoyote. Mtu kama huyu ima ni kutokana na kuwepo kasoro kwenye nia yake au kasoro katika ile njia ya kuitafuta. Ni lazima kwa mwanafunzi ajue njia sahihi ya kujifunza elimu.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016