Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Kutaendelea kutupwa ndani ya Moto mpaka pale useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Je, hakuna ziada yoyote?”[1]

mpaka al-Jabbaar aweke unyayo Wake juu yake ambapo utasema: “Tosha, tosha.”[2]?

MAELEZO

Hadiyth itakuja huko mbele:

“Kutaendelea kutupwa ndani ya Moto mpaka pale useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Je, hakuna ziada yoyote?”[3]

mpaka al-Jabbaar aweke unyayo Wake juu yake ambapo utasema: “Tosha, tosha.”

Bi maana umenitosha. Hadiyth inathibitisha kuwa Allaah yuko na unyayo na mguu kwa njia inayolingana na utukufu na ukubwa Wake. Atauweka juu ya Moto ambapo pasi na kudhurika, ambapo ulingane. Allaah ni muweza juu ya kila jambo na Moto ni kiumbe miongoni mwa viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Sisi tunaithibitisha Hadiyth kama ilivyokuja. Hatuingizi fahamu na akili zetu pungufu na hivyo tukamkanushia Allaah yale aliyojithibitishia Mwenyewe. Tunamthibitishia kuwa na unyayo, mguu na pia muundi, kama ilivyokuja katika Hadiyth. Hatupekui. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakuna chochote mfano Wake. Hatusemi kuwa viumbe pia wana sifa hizi na kwa hivyo tukizithibitisha basi tunamfananisha Allaah na viumbe. Kuna tofauti kati ya sifa za Allaah na sifa za viumbe Wake. Kwa kifupi ni kuwa sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala) zinalingana Naye wala hatujikakami katika suala hilo.

[1] 50:30

[2] al-Bukhaariy (4848), Muslim (2188) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 92-93.

[3] 50:30

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 24/07/2024