Miongoni mwa dalili hizo ni:

26 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia kijakazi:

“Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Juu mbinguni.” Akamuuliza tena: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”[1]

Ameipokea Abu Hurayrah, Mu´aawiyah bin al-Hakam, Muhammad bin ash-Shariyd na Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhum).

27 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hivi kweli hamniamini ilihali naaminiwa na Yule aliye mbinguni? Najiwa na khabari za mbinguni asubuhi na jioni.”[2]

Ameipokea Muslim.

28 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ya kwamba hakuna mwanaume anayemwita mke wake kitandani mwake ambapo akamkatalia, isipokuwa Yule ambaye yuko mbinguni anamkasirikia mpaka pale atapomuwia radhi.”[3]

Ameipokea Muslim.

29 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wakati Ibraahiym alipotupwa ndani ya moto alisema: ”Ee Allaah! Hakika Wewe uko Mmoja pekee juu ya mbingu na mimi ni mmoja pekee ardhini ninayekuabudu.”

Cheni ya wapokezi ni nzuri.

30 – Abu Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye atahisi maumivu mmoja wenu, au akahisi maumivu ndugu yake, aseme: “Mola wetu ni Allaah ambaye yuko mbinguni. Limetakasika jina Lako. Amri Yako iko mbinguni na ardhini kama ambavyo huruma Yako iko mbinguni. Tusamehe madhambi na makosa yetu. Wewe ni Mola wa wazuri. Teremsha rehema Yako na dawa Yako kwa huyu anayehisi maumivu.” ili aweze kupona.”[4]

Ameipokea Abu Daawuud.

[1] Kitaab-ul-Iymaan, uk. 36. al-Albaaniy amesema:

“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Muslim ameipokea kupitia njia ya mtunzi wa kitabu na pia kupitia njia zingine.” (Kitaab-ul-Iymaan, uk. 36)

[2] al-Bukhaariy (3610, 3344, 4351 na 7433), Muslim (1064) na Abu Daawuud (4764).

[3] al-Bukhaariy (5194) na Muslim (1436). Tamko ni la Muslim.

[4] Abu Daawuud (3892), an-Nasaa’iy (10877) na al-Haakim (1/344). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3892).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 50-53