07. Swalah isiyo na unyenyekevu ni kama mwili usiyo na roho

Vivyo hivyo kukosa unyenyekevu ndani ya swalah na kuhudhurisha moyo ndani yake mbele ya Mola Mtukufu (Tabaarak wa Ta´ala), ambaye hiyo ndiyo roho yake na kiini chake. Basi swalah isiyo na unyenyekevu wala kuhudhurisha moyo ni kama mwili wa maiti usio na roho ndani yake. Je, haoni haya mja kumpa kiumbe mfano wake zawadi ya mtumwa aliyekufa au kijakazi aliyekufa? Ni ipi dhana ya mja huyu kwa yule anayemkusudia kwa zawadi hiyo miongoni mwa mfalme, kiongozi au mwingine yeyote? Hali hii ya swalah ya kufikirika isiyo na unyenyekevu wala kuhudhurisha moyo na wala kukusanya hima kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani yake, ni sawa na hali ya huyu mtumwa au kijakazi aliyekufa ambaye mtu anataka kumpelekea mmoja wa wafalme. Kwa sababu hiyo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) haikubali kutoka kwake, hata kama inamvua faradhi kwa hukumu za kidunia, lakini hamlipi thawabu yoyote juu yake. Hakika mja hana katika swalah yake isipokuwa kile alichokielewa tu katika swalah hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mja huswali swalah na haandikiwi kwake isipokuwa nusu yake, theluthi yake, robo yake au khumsi yake” mpaka akasema ”au moja ya kumi yake”.”[1]

Inapasa kufahamu kuwa matendo yote hupitia njia hii. Kutofautiana kwa matendo mbele ya Allaah (Ta´ala) ni kwa tofauti ya yaliyomo katika nyoyo ya imani, ikhlaasw, mapenzi na yanayofuatia hayo.

[1] Abu Daawuud (786), an-Nasaa’iy katika “al-Kubraa” (614-615) na Ahmad (6/408-409). Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (1889), al-´Iraaqiy katika “al-Mughniy” (1/120) na al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (796).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 29/07/2025