Alama ya kutukuza kwa amri ni kuzingatia nyakati zake, mipaka yake, kuchunguza nguzo zake, wajibu wake na ukamilifu wake, kujishughulisha kuitekeleza katika wakati wake, kufanya haraka kuiendea inapowajibika, huzuni na majonzi na majuto yanapopitwa na haki ya miongoni mwa haki zake, kama vile mtu anavyohuzunika kwa kupitwa na swalah ya mkusanyiko huku akijua kuwa swalah yake peke yake imekubaliwa, lakini amepitwa na ujira wa mara ishirini na saba. Lau mtu anayejishughulisha na biashara na mauzo akipitwa na dili moja tu katika mji wake bila safari wala mashaka, yenye thamani ya dinari ishirini na saba, hakika angejiuma mikono kwa majuto na huzuni. Basi vipi hali ya yule aliyepitwa na ujira wa mara ishirini na saba, ambapo kila moja kati ya hizo ni bora kuliko elfu na elfu ya elfu na kadiri Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atakavyo. Basi mja anapojipotezea faida hii basi amefilisika. Wanazuoni wengi wanasema kuwa mtu anayeswali bila kujali kisha isitoshe moyo wa baridi na hana huzuni kwa msiba huu wala hajaingiwa na khofu, halipwi kwa swalah yake. Kwa sababu huko kunajulisha kutokutukuza amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika moyo wake.
Vilevile ikiwa amekosa mwanzo wa wakati ambao ni radhi ya Allaah (Ta´ala), au amekosa safu ya kwanza ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamsifia na Malaika Wake kumuombea msamaha, lau mja angejua fadhilah yake basi angepigania juu yake kwa kupigana na ijapo ingelikuwa kwa kupiga kura.
Vivyo hivyo kukosa mkusanyiko mkubwa wa watu ambao swalah huongezewa ujira kwa wingi au uchache wake. Kadiri watu wanavyoongezeka ndivyo inavyopendeza zaidi na Allaah (´Azza wa Jall) na kadiri hatua zinavyokuwa ndefu, kila hatua humfutia dhambi na nyingine humpandisha juu daraja.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 16-17
- Imechapishwa: 29/07/2025
Alama ya kutukuza kwa amri ni kuzingatia nyakati zake, mipaka yake, kuchunguza nguzo zake, wajibu wake na ukamilifu wake, kujishughulisha kuitekeleza katika wakati wake, kufanya haraka kuiendea inapowajibika, huzuni na majonzi na majuto yanapopitwa na haki ya miongoni mwa haki zake, kama vile mtu anavyohuzunika kwa kupitwa na swalah ya mkusanyiko huku akijua kuwa swalah yake peke yake imekubaliwa, lakini amepitwa na ujira wa mara ishirini na saba. Lau mtu anayejishughulisha na biashara na mauzo akipitwa na dili moja tu katika mji wake bila safari wala mashaka, yenye thamani ya dinari ishirini na saba, hakika angejiuma mikono kwa majuto na huzuni. Basi vipi hali ya yule aliyepitwa na ujira wa mara ishirini na saba, ambapo kila moja kati ya hizo ni bora kuliko elfu na elfu ya elfu na kadiri Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atakavyo. Basi mja anapojipotezea faida hii basi amefilisika. Wanazuoni wengi wanasema kuwa mtu anayeswali bila kujali kisha isitoshe moyo wa baridi na hana huzuni kwa msiba huu wala hajaingiwa na khofu, halipwi kwa swalah yake. Kwa sababu huko kunajulisha kutokutukuza amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika moyo wake.
Vilevile ikiwa amekosa mwanzo wa wakati ambao ni radhi ya Allaah (Ta´ala), au amekosa safu ya kwanza ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamsifia na Malaika Wake kumuombea msamaha, lau mja angejua fadhilah yake basi angepigania juu yake kwa kupigana na ijapo ingelikuwa kwa kupiga kura.
Vivyo hivyo kukosa mkusanyiko mkubwa wa watu ambao swalah huongezewa ujira kwa wingi au uchache wake. Kadiri watu wanavyoongezeka ndivyo inavyopendeza zaidi na Allaah (´Azza wa Jall) na kadiri hatua zinavyokuwa ndefu, kila hatua humfutia dhambi na nyingine humpandisha juu daraja.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 16-17
Imechapishwa: 29/07/2025
https://firqatunnajia.com/06-je-wewe-unatukuza-maamrisho-ya-allaah/