Ukishazitambua Hadiyth hizi basi hakika utaona kuwa ni hoja yenye kukata mizozo kabisa juu ya kwamba Sunnah ni kuswali swalah zote mbili za ´Iyd sehemu ya uwanja. Haya ndio maoni ya wanachuoni wengi. Imaam al-Baghawiy amesema katika “Sharh-us-Sunnah”:

“Sunnah ni Imaam kutoka uwanjani. Ikiwa kutakuwa na udhuru wowote, basi ataswali mskitini.”[1]

Msikiti ulioko ndani ya mji.

Imaam Muhyiy-ud-Diyn an-Nawawiy amesema katika pindi alipokuwa akizungumzia Hadiyth ya kwanza:

“Hii ni dalili kwa mwenye kusema kuwa imependekezwa kuswali swalah ya ´Iyd mahali pa uwanja na kwamba ni bora kuliko kufanya hivo msikitini. Kitendo hichi ndicho kinachofanywa na watu katika miji mingi. Kuhusiana na watu wa Makkah, walikuwa ni wenye kuiswali msikitini tangu hapo mwanzo. Wenzetu wana mitazamo miwili juu ya suala hili:

1- Bora ni kuswali jangwani, kutokana na Hadiyth hii.

2- Bora ni msikitini ikiwa hakuna kujibana. Maoni haya ndio sahihi zaidi kwa wengi. Wamesema kwamba sababu iliyowapelekea watu wa Makkah kuswali msikitini ni kutokana na upana wake na pia sababu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sehemu ya uwanja, ilikuwa ni kwa sababu msikitini kulikuwa na kujibana. Ni dalili inayofahamisha kuwa lililo bora ni kuswali msikitini ikiwa kuna sehemu ya kutosha.”[2]

[1] Haya yamesemwa na Shaykh ´Aliy al-Qaariy katika “al-Mirqaat” (02/245). Tazama “Sharh-us-Sunnah” (04/294), al-Maktab al-Isaamiy kwa chapa ya Shu´ayb Arnaauutw kwa uhakiki wa Zuhayr ash-Shaawaysh.

[2] Sharh Swahiyh Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 13/05/2020