Watu wako katika ngazi tatu:

1- Mjinga.

2- Mwanachuoni mzembe.

3- Mwanachuoni mkaidi.

Hatuwezi kumlinganisha kila mmoja na mwingine. Ni lazima kila mmoja kumtteremsha ngazi yake. Kwa ajili hii pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Mu´aadh kwenda Yemen alimwambia:

“Hakika wewe unawaendea watu katika Ahl-ul-Kitaab.”

Alimwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hivo ili Mu´aadh aweze kujua hali yao na ajiandae kwa yale yanayopelekea hali hii na vilevile awazungumzishe kwa yale yanayopelekea hali hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017