Sahl bin Sa’d ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna pazia sabini elfu ya nuru chini ya Allaah na giza. Hapana nafsi yoyote inayopenya kupitia pazia hizo kwa sauti yoyote, isipokuwa roho yake huteketea.”
Ameipokea Abu Ya´laa al-Mawsuliy katika ”al-Musnad” yake na al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”.
´Imraan bin Huswayn amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Zipokeeni khabari njema, ee Banuu Tamiym!” Wakasema: ”Umetubashiria, hivyo tupe basi!” Akasema: ”Zipokeeni khabari njema, enyi watu wa Yemen!” Wakasema: ”Umetubashiria, basi hebu tueleze jambo zima lilianzaje!” Akasema: ”Allaah alikuwa juu ya ´Arshi na alikuwa kabla ya kila kitu. Akaandika kwenye Ubao kila kitu kitachokuwa.”[1]
Swahiyh.
Anas amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiondosha nguo yake kutoka mabegani ili maji yampate, na akisema: ”Ndio punde imetoka kwa Mola wake.”[2]
Ameipokea Muslim.
Ameeleza tena ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Panapokuwa ni siku ya ijumaa, Allaah (´Azza wa Jall) hushuka kutoka juu hadi kwenye Kursiy Yake. Kisha Kursiy inazungukwa na mimbari za nuru. Kisha wanakuja Manabii ili kukaa juu yake. Kisha huzungukwa tena na viti vya dhahabu. Kisha wanakuja wakweli na mashahidi ili kukaa juu yake. Kisha wanakuja wakazi wa Peponi ili kukaa juu ya vitanda. Hapo ndipo Mola wao (´Azza wa Jall) hujionyesha kwao ili wapate kuangalia uso Wake. Yeye ndiye anayesema: ”Mimi ndiye niliyewatimizia ahadi Yangu, hivyo basi niombeni.” Basi watamwomba mpaka matamanio yao yatimie. Ndipo watafunguliwa yale ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia na wala havikuwahi kuingia moyoni mwa mwanadamu ambayo ni sawa na muda watu kurudi kutoka ijumaa. Kisha hupanda tena juu ya Kursiy Yake na wakweli na mashahidi wakapanda pamoja Naye.”
Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”[3] na Haafidhw Abu Ahmad al-´Assaal.
[1] al-Bukhaariy (7418).
[2] Muslim (898).
[3] as-Sunnah (460).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 40-41
- Imechapishwa: 21/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 40-41
Imechapishwa: 21/12/2025
https://firqatunnajia.com/07-namna-kilivyoanza-kila-kitu/