Kwa mfano Suufiyyah wenzetu katika Uislamu wamo katika njia ya manaswara. Wanamuabudu Allaah, wanaipa kisogo dunia na wanawaepuka watu, lakini hata hivyo hawana elimu. Hawasomi, bali wanaidharau elimu. Wanawaambia watu wafanye matendo na wanaona ni vipi elimu itamshughulisha mtu na kufanya matendo. Wanaona kuwa kinachotakikana kutoka kwa watu ni kufanya matendo. Wanawapuuzisha watu na suala la kutafuta elimu, kukaa kwa wanazuoni na kuchukua elimu kutoka kwao. Wanawatuhumu tuhumu mbalimbali wale wenye kujishughulisha na kutafuta elimu na kwamba wameacha kufanya matendo. Hili ni mosi.
Pili wanasema kuwa elimu haiji kwa kusoma. Badala yake wanaona kuwa elimu inamjia mtu namna hii tu! Wanaona kuwa pindi mtu atajishughulisha na ´ibaadah Allaah atamtunukia elimu bila hata ya kujifunza. Huu ni upotofu.
Tutadhari na jambo hili. Elimu inakuja kwa kusoma. Huwezi kuifikia elimu isipokuwa njia ya kusoma kupitia kwa wanazuoni. Elimu inatangulia mbele kabla ya kuzungumza na kutenda. Imaam al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy:
Mlango: “Elimu inatangulia kabla ya kauli na kutenda.”
Kisha akataja Aayah ifuatayo:
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
“Basi jua ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na za waumini wanaume na waumini wanawake.”[1]
Kwanza unatakiwa kutambua kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Hili linapatikana kwa mtu kusoma, halafu baada ya hapo ndio aombe msamaha na kutenda. Kwa hivyo ni lazima kwa mtu kusoma. Elimu ndio ndio inayokujulisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´a). Allaah ameteremsha Kitabu na amemtuma Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili atuelekeze katika Njia sahihi ambayo tutapita juu yake; nayo ni elimu yenye manufaa na matendo mema.
[1] 47:19
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, uk. 29-32
- Imechapishwa: 06/05/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, uk. 29-32
Imechapishwa: 06/05/2024
https://firqatunnajia.com/07-mfumo-wa-suufiyyah-ni-kama-wa-manaswara/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)