17 – Bishr bin Muhammad ametuhadithia: ´Abdullaah ametukhabarisha: Muhammad bin Shu´ayb ametuhadithia: ´Umar bin Yaziyd an-Naswriy amenihadithia, kutoka kwa Abu Sallaam, ambaye amemukhabarisha kutoka kwa Abu Umaamah al-Baahiliy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Watu aina tatu Allaah hakubali chochote kile kutoka kwao: mwasi wazazi, anayeeneza umbea na anayekadhibisha makadirio.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 116
  • Imechapishwa: 29/12/2024