Jambo lingine muhimu ni vipi kunathibiti kuingia kwa Ramadhaan. Ramadhaan inathibiti kwa muislamu mmoja kuapa kwa Allaah ya kwamba ameona mwezi mwandamo. Pindi hili litawekwa hadharani basi itakuwa ni lazima kufunga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Fungeni pindi mtapouona na fungueni pindi mtapouona. Iwapo mtafunikwa na wingu kamilishe thelathini.”[1]
Bi maana timizeni siku thelathini. Uonekanaji huu unawahusu wale wote wanaoeshi huko. Kwa mfano mwezi mwandamo ukionekana Pakistan, ´Iraaq, Kuwait au karibu na nchi za karibu yetu, basi inatulazimu kufunga. Kwa sababu jua linazama kwao kabla yetu. Mwezi mwandamo ukithibiti kwao kwa kuonekana, inatulazimu kufunga. Na ukithibiti kwetu kwa kuonekana, inalazimu nchi zilizo karibu yetu, kama mfano wa Misri na nchi zingine za Afrika, kufunga. Kuzama kwa jua katika nchi hizo kunakuwa baada yetu. Haya ndio maoni ya haki ninayoonelea.
Kuna waislamu wenye kusema mwezi mwandamo ukionekana katika nchi fulani, basi ni lazima waislamu wote kufunga kutokana na muonekano huo. Maoni haya yalikuwa kabla ya kubainika kuwa kuzama kwa jua kunatofautiana katika miji. Watu walikuwa wakitilia shaka tofauti hii kabla ya teknolojia ya kisasa kufanya kazi. Leo mambo yamekuwa wazi kabisa. Kila mji unajua ni lini jua lazama. Ni kitu kinachojulikana kupitia vyombo vya khabari na saa. Leo imejulikana kuwa kuzama kwa jua kunatofautiana.
Mwezi mwandamo ukionekana katika mji, basi ni lazima kwa miji ilio baada ifunge kwa sababu kuzama kwa jua katika nchi hiyo kunatokea kabla ya nchi hizo zingine.
Muonekano ni lazima uwe kwa macho. Unatakiwa uwe wa kawaida, na sio kwa kutumia mitambo. Muonekano wa kutumia mitambo huakubaliwi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sisi ni Ummah usiokuwa wa kiusomi; hatuandiki na wala hatusomi. Mwezi uko namna hii na namna hii.”[2]
Bi maana wakati fulani ni siku ishirini na tisa na wakati mwingine ni siku thelathini.
[1] al-Bukhaariy (1909) na Muslim (1081).
[2] al-Bukhaariy (1913) na Muslim (1080).
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Istiqbaal Shahri Ramadhwaan, uk. 37-39
- Imechapishwa: 09/06/2017

Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Istiqbaal Shahri Ramadhwaan, uk. 37-39
Imechapishwa: 09/06/2017
https://firqatunnajia.com/07-kuthibiti-kwa-kuingia-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)