Wale wanaoonelea kufaa kuhuisha Bid´ah hii wanaweza kushikilia hoja dhaifu zaidi kuliko nyumba ya buibui. Hoja hizo zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo:
1 – Wanadai kuwa kwa kufanya hivo wanamtukuza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunajibu hilo kwa kusema kwamba kumtukuza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inakuwa kwa kumtii, kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake na kumpenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), sio kumtukuza kwa mambo ya Bid´ah, ukhurafi na maasi. Yote haya tuliyoyata yanapatikana katika sherehe za mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu ni kitendo cha madhambi.
Watu waliokuwa wakimuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa upeo wa hali ya juu ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). ´Urwah bin Mas´uud alisema kuwaambia Quraysh:
“Enyi watu! Naapa kwa Allaah kwamba nimekwenda kwa wafalme, kwa Qaysar, Kisraa na an-Najaashiy. Napaa kwa Allaah sijawahi kuona mfalme yeyote anayetukuzwa na wafuasi wake kama anavyotukuzwa Muhammad na Maswahabah wake. Naapa kwa Allaah hakutoa makozi isipokuwa yalianguka kwenye kiganja cha mmoja wao akajipaka usoni na ngozi yake. Alipowaamrisha waliharakia kutekeleza amri yake. Alipowatawadha walikaribiana kugombana juu ya maji yake. Alipoongea walishusha sauti zao mbele yake. Wala hawakumkazia macho kutokana na kule kumtukuza.”[1]
Licha ya matukuzo yote haya hawakufanya siku ya kuzaliwa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakufanya kuwa sikukuu na sherehe. Lau jambo hilo ingelikuwa limewekwa katika Shari´ah, basi wasingeliacha.
[1] al-Bukhaariy (03/178) (nr. 2731, 2732) pamoja na al-Fath (05/388).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 151-152
- Imechapishwa: 06/09/2025
Wale wanaoonelea kufaa kuhuisha Bid´ah hii wanaweza kushikilia hoja dhaifu zaidi kuliko nyumba ya buibui. Hoja hizo zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo:
1 – Wanadai kuwa kwa kufanya hivo wanamtukuza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunajibu hilo kwa kusema kwamba kumtukuza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inakuwa kwa kumtii, kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake na kumpenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), sio kumtukuza kwa mambo ya Bid´ah, ukhurafi na maasi. Yote haya tuliyoyata yanapatikana katika sherehe za mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu ni kitendo cha madhambi.
Watu waliokuwa wakimuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa upeo wa hali ya juu ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). ´Urwah bin Mas´uud alisema kuwaambia Quraysh:
“Enyi watu! Naapa kwa Allaah kwamba nimekwenda kwa wafalme, kwa Qaysar, Kisraa na an-Najaashiy. Napaa kwa Allaah sijawahi kuona mfalme yeyote anayetukuzwa na wafuasi wake kama anavyotukuzwa Muhammad na Maswahabah wake. Naapa kwa Allaah hakutoa makozi isipokuwa yalianguka kwenye kiganja cha mmoja wao akajipaka usoni na ngozi yake. Alipowaamrisha waliharakia kutekeleza amri yake. Alipowatawadha walikaribiana kugombana juu ya maji yake. Alipoongea walishusha sauti zao mbele yake. Wala hawakumkazia macho kutokana na kule kumtukuza.”[1]
Licha ya matukuzo yote haya hawakufanya siku ya kuzaliwa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakufanya kuwa sikukuu na sherehe. Lau jambo hilo ingelikuwa limewekwa katika Shari´ah, basi wasingeliacha.
[1] al-Bukhaariy (03/178) (nr. 2731, 2732) pamoja na al-Fath (05/388).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 151-152
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/07-kusherehekea-maulidi-ni-kumtukuza-mtume/