Ambaye atakula kwa udhuru kisha ukamwondoka udhuru wake katikati ya mchana wa Ramadhaan – mfano wa watu hao ni msafiri aliyefika kutoka safarini, mwenye hedhi na nifasi waliosafika, kafiri anaposilimu, mwendawazimu anapopata fahamu na mdogo anapobaleghe – basi wanatakiwa kujizuia sehemu ile ya mchana iliyobakia na baadaye watalipa. Vivyo hivyo kuthibitisha ushahidi wa kuingia mwezi katikati ya mchana, basi waislamu wanatakiwa kujizuia ile sehemu ya mchana iliyobakia na baadaye watalipa baada ya Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/377)
  • Imechapishwa: 27/03/2021