30 – Inatakiwa kuwasikiliza na kuwatii viongozi katika yale Allaah anayoyapenda na kuyaridhia. Mwenye kutawalia ukhalifa baada ya watu kuafikiana juu yake na kuridhika naye, basi huyo ni Kiongozi wa waumini.
31 – Haijuzu kwa yeyote kulala japo usiku mmoja na hali ya kuwa haonelei kuwa ana kiongozi juu yake, ni mamoja awe ni mwema au mtenda maovu.
32 – Hijjah na vita vitaendelea kuwepo pamoja na kiongozi. Swalah ya ijumaa nyuma yao inajuzu. Baada ya hapo ataswali Rak´ah sita, atazipambanua baina ya kila Rak´ah mbili, hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal.
33 – Ukhalifah utaendelea kuwa haki ya Quraysh mpaka pale ataposhuka ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam).
34 – Atayefanya uasi dhidi ya kiongozi mmoja wapo wa waislamu ni Khaarijiy. Atakuwa ameugawa umoja wa waislamu, ameenda kinyume na mapokezi na kifo chake ni kifo cha kipindi kabla ya kuja Uislamu.
35 – Haijuzu kumpiga vita mtawala na kufanya uasi dhidi yao hata kama watafanya dhuluma. Haya ni kutokana maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwambia Abu Dharr al-Ghifaariy:
“Kuwa na subira hata kama atakuwa ni mja wa kihabeshi.”[1]
Vilevile aliwaambia Wanusuraji:
“Kuweni na subira mpaka mtapokutana nami kwenye Hodhi.”[2]
Si katika Sunnah kumpiga vita mtawala. Hakika ni jambo ambalo ndani yake lina maharibifu ya dini na dunia.
36 – Ni halali kuwapiga vita Khawaarij endapo watawavamia waislamu mali zao, maisha yao na familia zao. Hata hivyo haifai ikiwa watakimbia kuwatafuta. Mtu asiwaue wajeruhi wao, asichukue ngawira zao, asiwaue mateka wao na asiwafuate wale wenye kukimbia.
37 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba haifai kumtii mtu yeyote katika kumuasi Allaah (´Azza wa Jall).
[1] Muslim (1837), Ahmad (3/171) na Ibn Maajah (2862).
[2] al-Bukhaariy (7057) na Muslim (1845).
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 78-79
- Imechapishwa: 17/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 78-79
Imechapishwa: 17/12/2024
https://firqatunnajia.com/07-kumsikiliza-na-kumtii-kiongozi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)