07. Hapa ndipo tafsiri zote za Salaf zinakuwa sahihi

Miongoni mwa ikhtilafu zao ni kwamba masimulizi yao yanaweza kuleta tafsiri ya vitu viwili, ima kwa sababu neno hilo linaweza kuwa na maana zote mbili, kwa mfano wa neno (قَسْوَرَة) lenye maana ya mpiga mishale na simba na kitenzi (عَسَعسَ) lenye maana ya kuja kwa usiku na kuondoka kwake, au kwa sababu neno hilo maana yake kimsingi ni kitu kimoja lakini inaweza kurejelea moja ya aina mbili au moja ya vitu viwili, kama kiwakilishi katika maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ

”… kisha akakurubia na akashuka, kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.”[1]

Mfano mwingine ni maneno Yake (Ta´ala):

وَالْفَجْرِ وَلَيَالٍ عَشْرٍ

”Naapa kwa Alfajiri.Na Naapa kwa masiku kumi!”[2]

Wakati fulani inawezekana kwamba tafsiri zote za Salaf ni sahihi, na wakati mwingine isiwe hivyo. Inawezekana ikiwa Aayah imeteremshwa mara mbili. Katika hali hiyo kukakusudiwa jambo moja wakati fulani na jambo lingine wakati mwingine. Inawezekana pia ikiwa neno lina maana zaidi ya moja. Hayo ndio maoni ya kikosi kikubwa katika wanazuoni wa Maalikiyyah, Shaafi’iyyah na Hanaabilah pamoja na wengi katika wanazuoni wa falsafa. Isitoshe inawezekana ikiwa neno lina maana ya kitu kimoja na kwa hivyo ni la jumla kwani hakuna uainishaji wa lazima. Ikiwa aina hii imesihi kuwa inakusanya maono mawili, basi ni katika sampuli ya pili.

[1] 53:8-9

[2] 89:1-2

  • Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 25/03/2025