Kutokana na yaliyotangulia inapata kuwa wazi ya kwamba hakuna nafasi kabisa kwa yeyote yule – pasi na kujali ubobeaji wake katika lugha ya kiarabu na adabu zake – kuifahamu Qur-aan tukufu pasi na kutaka msaada kwa hilo kutoka katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) za kimaneno na za kimatendo. Hakuna watu waliokuwa wamebobea katika lugha ya kiarabu kuliko Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Qur-aan imeteremshwa kwa lugha yao na walikuwa hawajaingiliwa na uchafu wa uajemi, upofu na utamkaji wa kimakosa. Pamoja na hivyo walikosea katika kuielewa Aayah iliyotangulia pindi walipotegemea lugha yao peke yake. Kujengea juu ya hili pindi mtu anapokuwa mjuzi zaidi wa lugha ndipo anasalimika zaidi kuielewa Qur-aan na kutoa hukumu kutoka kwayo kuliko yule ambaye hayuko hivo. Vipi kuhusu yule asiyeitegemea au akawa kimsingi yeye haijali kabisa? Kwa ajili hiyo miongoni mwa kanuni ambazo ni zenye kutegemewa kwa wanachuoni ni Qur-aan kuifasiri kwa Qur-aan na Sunnah, kisha Qur-aan kuifasiri kwa maneno ya Maswahabah na kadhalika.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam, uk. 15-16
- Imechapishwa: 10/02/2017
Kutokana na yaliyotangulia inapata kuwa wazi ya kwamba hakuna nafasi kabisa kwa yeyote yule – pasi na kujali ubobeaji wake katika lugha ya kiarabu na adabu zake – kuifahamu Qur-aan tukufu pasi na kutaka msaada kwa hilo kutoka katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) za kimaneno na za kimatendo. Hakuna watu waliokuwa wamebobea katika lugha ya kiarabu kuliko Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Qur-aan imeteremshwa kwa lugha yao na walikuwa hawajaingiliwa na uchafu wa uajemi, upofu na utamkaji wa kimakosa. Pamoja na hivyo walikosea katika kuielewa Aayah iliyotangulia pindi walipotegemea lugha yao peke yake. Kujengea juu ya hili pindi mtu anapokuwa mjuzi zaidi wa lugha ndipo anasalimika zaidi kuielewa Qur-aan na kutoa hukumu kutoka kwayo kuliko yule ambaye hayuko hivo. Vipi kuhusu yule asiyeitegemea au akawa kimsingi yeye haijali kabisa? Kwa ajili hiyo miongoni mwa kanuni ambazo ni zenye kutegemewa kwa wanachuoni ni Qur-aan kuifasiri kwa Qur-aan na Sunnah, kisha Qur-aan kuifasiri kwa maneno ya Maswahabah na kadhalika.
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam, uk. 15-16
Imechapishwa: 10/02/2017
https://firqatunnajia.com/07-hakuna-yeyote-awezaye-kuifahamu-qur-aan-kwa-kutegemea-ubobeaji-wake-wa-lugha-ya-kiarabu-peke-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)