07. Hadiyth “Hakuna mwanamume anayeoga siku ya ijumaa, akajitwaharisha… “

689- Salmaan al-Faarisiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mwanamume anayeoga siku ya ijumaa, akajitwaharisha kiasi na anavyoweza, anajitia mafuta na manukato nyumbani kwake halafu akatoka pasi na kutenganisha kati ya mambo mawili, akaswali kiasi na alichoandikiwa na akanyamaza pale imamu anapoanza kuzungumza, isipokuwa husamehewa yaliyoko baina yake na baina ya ijumaa nyingine.[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy[2]. Katika upokezi wa an-Nasaa´iy imekuja:

“Hakuna mwanaume anayejitwaharisha siku ya ijumaa kama alivyoamrishwa kisha akatoka nyumbani kwake mpaka akafika katika swalah ya ijumaa na akanyamaza mpaka akatimiza swalah yake, isipokuwa hufutwa yale yote yaliyokuwa katika ijumaa kabla yake.”[3]

at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa mlolongo wa wapokezi mzuri Hadiyth inayofanana na upokezi uliyoko kwa an-Nasaa´iy ambapo mwisho wake kuna:

“… isipokuwa hufutwa yale yote kati yake na ijumaa inayokuja midhali kutaepukwa yale madhambi makubwa.”

[1] Swahiyh.

[2] Nzuri na Swahiyh. Bi maana katika ”as-Sunan al-Kubraa” (1664) na (1724). al-Haakiy ameipokea pia na kusema:

”Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.” (01/277).

[3] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/432)
  • Imechapishwa: 17/02/2017