06. Yule anayependwa zaidi na Allaah humfanya asitambulike

30 – Ahmad bin ´Iysaa al-Miswriy amenihadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin al-Haarith na Ibn Lahiy´ah, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Sinaan bin Sa´d, kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Inatosha kuoneysha uovu wa mtu, isipokuwa yule ambaye amekingwa na (´Azza wa Jall), kuwa watu wamuelekezea vidole katika dini yake na dunia yake.”

31 – Ishaaq bin al-Bahluul at-Tanuukhiy ametuhadithia: Ibn Abiy Fudayk ametuhadithia: Muhammad bin Sulaymaan al-Akhnasiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Waahid bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inatosha kuoneysha uovu wa mtu, isipokuwa yule ambaye amekingwa na (´Azza wa Jall), kuwa watu wamuelekezea vidole katika dini yake na dunia yake. Hakika Allaah hatazami sura zenu; lakini anazitazama nyoyo na matendo yenu.”

32 – ´Aliy bin al-Ja´d ametuhadithia: al-Mubaarak bin Fadhwaalah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, aliyeeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inatosha kuoneysha uovu wa mtu watu wanamuelekezea vidole katika dini yake na dunia yake.”

33 – Abun-Naswr al-Mu-addib amenihadithia: Daawuud bin al-Muhabbir ametuhadithia, kutoka kwa al-Mubaarak bin Fadhwaalah, ambaye amesema:

”Tulimwambia al-Hasan: ”Ee Abu Sa´iyd, hakika watu wakikuona wanakuashiria kwa vidole.” Akasema: ”Si hicho kilichokusudiwa hapa. Hakika hapana vyenginevyo kilichoksudiwa ni mzushi katika dini yake na fasiki katika dunia yake.”­

34 – Baba yangu amenihadithia: Ibraahiym bin Hiraasah ametuhadithia, kutoka kwa al-Quraah, kutoka kwa mzee mmoja kutoka Ahnaf, ambaye ameeleza kuwa amemsikia ´Aliy akisema:

“Jidunike, acha kujulikana. Usijiinue mwenyewe ukatajwa na hivyo ukatambulika. Kithirisha kukaa kimya utasalimika, wafurahishe wema na wachukize waovu.”

35 – Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia: Ahmad bin Kurduus ametuhadithia: Makhlad bin al-Husayn ametuhadithia, kutoka kwa Abu Bakr bin al-Fadhwl: Nimemsikia Ayyuub akisema:

“Hakuna hatokuwa mkweli na Allaah isipokuwa hufurahi asijulikane mahali alipo.”

36 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia alHasan bin ar-Rabiy´: Sa´iyd bin ´Abdul-Ghaffaar amenihadithia:

”Nilikuwa mimi na Muhammad bin Yuusuf al-Aswbahaaniy wakati alipofikiwa na barua ya Muhammad bin al-´Alaa bin al-Musayyab kutoka Baswrah. Muhammad bin Yuusuf akaisoma na   kunambia: “Je huoni alichoniandikia Muhammad bin al-´Alaa?” Ndani yake mna haya: “Ee ndugu yangu kipenzi! Anayempenda Allaah basi hupenda asijulikane na watu.”

37 – Abu Bakr ash-Shaybaaniy amenihadithia: Nimemsikia Sufyaan bin ´Uyaynah akisema: Bishr bin Mansuur amenambia:

“Hakuna yeyote ambaye ataaibishwa Siku hiyo kiasi kwamba aibu yake ifichikane kwa yeyote.”

38 – Muhammad bin al-Jubayr amenihadithia: ´Abdul-Wahhaab bin ´Atwaa’ amenihadithia, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa Qataadah, ambaye amesema:

“Hakuna mtu ataaibishwa Siku hiyo kiasi kwamba aibu yake ifichikane kwa yeyote.”

39 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia:

“Nimemwona ath-Thawriy katika usingizi, nikamwambia: ”Niusie.” Akasema: ”Punguza kujulikana na watu.”

40 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, aliyesimulia kwamba Sammaak bin Salamah amesema:

“Ewe moyo, jihadhari na kuwa na marafiki wengi!”

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 55-68
  • Imechapishwa: 22/01/2026