06. Tafsiri ya Tawhiyd na kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah

 1- Allaah (Ta´ala) amesema:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza.” (17:57)

2-

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ

”Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]! [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumba, basi hakika Yeye ataniongoa.” (43:26-28)

3-

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ

”Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni waungu badala ya Allaah.” (09:31)

4-

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ

”Wapo katika watu ambao wanafanya badala ya Allaah washirika [na] wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.” (02:165)

5- Katika Swahiyh imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Atakayesema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah, basi imeharamika mali na damu yake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jall).”

Maelezo kuhusu mlango huu na ile milango mingine ilio baada yake ndani yake kumetajwa mambo makubwa na ya muhimu. Nayo ni tafsiri ya Tawhiyd na tafsiri ya shahaadah ambayo yamefasiriwa kwa njia ya wazi kabisa.

Katika hayo ni Aayah ya Suurah al-Israa´ ambayo imewaraddi washirikina ambao wanawaomba waja wema. Imebainisha ya kwamba hii ndio shirki kubwa.

Katika hayo ni Aayah ya Suurah al-Baraa´ inayobainisha ya kwamba watu wa Kitabu waliwafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni waungu badala ya Allaah. Allaah amebainisha vilevile ya kwamba hakuwaamrisha jengine isipokuwa wamuabudu Mungu Mmoja. Haya pamoja na kuwa tafsiri ya Aayah isiyokuwa na utatizi ndani yake inahusiana na kuwaabudu wanachuoni na waja wema katika maasi na kwamba hawakuwaomba.

Katika hayo ni maneno ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kwa makafiri:

إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي

“Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]! [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumb.”

Kwa vile vyote vinavyoabudiwa amemvua Mola Wake. Allaah (Subhaanah) ameeleza kuwa chuki hii na mapenzi haya ndio tafsiri ya shahaadah na kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na akasema:

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Na akalifanya ni neno lenye kubakia katika kizazi chake ili [wale wanaopinda kutoka katika ile imani safi] wapate kurejea.” (43:28)

Katika hayo ni Aayah ya Suurah al-Baqarah inayohusiana na makafiri ambao Allaah (Ta´ala) amesema juu yao:

وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ

“Wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.” (02:167)

Ametaja namna ambavyo wanawapenda washirika wao kama wanavyompenda Allaah. Haya yanafahamisha ya kwamba wao walikuwa na mapenzi makubwa kabisa. Pamoja na hivyo hayakuwafanya kuwa waislamu. Vipi kuhusu yule ambaye anampenda mshirika zaidi kuliko anavyompenda Allaah? Vipi kuhusu yule ambaye hampendi isipokuwa mshirika peke yake na akawa hampendi Allaah?

Katika hayo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayesema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah, basi imeharamika mali na damu yake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jall).”

Hadiyth hii ndio tafsiri bora kabisa iwezayo kufasiri maana ya hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Hakufanya kule kutamka tu ndio kunamsalimisha mtu maisha yake na damu yake. Wala kule kutambua, kukubali na kwamba hamuombi mwengine asiyekuwa Allaah pekee. Uhakika wa mambo ni kuwa mali na damu yake havisalimiki mpaka vilevile akanushe vile vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah. Iwapo atakuwa na mashaka au akanyamaza juu ya suala hili basi havisalimiki mali wala damu yake. Suala hili ni kubwa na tukufu zaidi. Ni jambo liko wazi kabisa. Ni hoja yenye kukata kabisa dhidi ya wapinzani.

MAELEZO

Hapa mwandishi amebainisha tafsiri ya Tawhiyd na kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah kwa njia inayoafikiana na matamshi yake na kuonyesha yanayopingana nayo. Kwa sababu mambo hufahamika kwa kinyume chake. Ametaja mlango huu ili uweze kuelewa uhakika wa Tawhiyd. Uhakika wake ni kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah na kumtekelezea aina zote Yeye. Unatakiwa kuamini hilo kwa moyo na kulitendea kazi kwa viungo vya mwili:

1-  Allaah (Ta´ala) amesema:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza.” (17:57)

Kabla ya hapo Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا

“Sema: “Iteni wale ambao mnadai [ni waabudiwa] badala ya Allah, basi [mtaona kuwa] hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha [kwa mwengine].” (17:56)

Kumuomba asiyeweza kumiliki kuondosha dhara wala kuleta manufaa badala ya Allaah ndio shirki na kinyume chake ndio Tawhiyd. Allaah anamwamrisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia wale wanaowaomba waungu wao badala ya Allaah kwa njia ya kuwakemea:

فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ

“… hawamiliki kukuondesheeni dhara… “

Bi maana aina zote za madhara.

وَلَا تَحْوِيلًا

“… na wala kuihamisha [kwa mwengine].”

Bi maana hawawezi kuhamisha dhara kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama kutoka kichwani kwenda miguuni. Hili ni kwa Allaah pekee ndiye awezaye kuondosha mara na kuleta manufaa. Allaah (Ta´ala) amesema:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza.” (17:57)

Anamaanisha wale wanaowaomba Malaika, Mitume na waja wema. Kwa ajili hiyo amesema:

يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ

“… wanatafuta kwa Mola wao njia… “

Bi maana pamoja na kuwa wale wanaoombwa ni wema hawamiliki kuondosha dhara wala kulihamisha. Ina maana kwamba masanamu mengine yote wana haki zaidi ya kutoweza kufanya hivo. Njia maana yake ni kujikurubisha kwa Allaah kwa utiifu. Wao wenyewe wanajitahidi kuwa karibu na Allaah kwa kufanya aina mbalimbali za utiifu.

وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ

“… wanataraji Rahmah Yake na wanakhofu adhabu Yake… ” (17:57)

Kwa sababu ni waja Wake. Wanamtarajia Yeye na wanamuogopa. Ni vipi basi wataombwa?

2-

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ

”Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]! [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumba, basi hakika Yeye ataniongoa.” (43:26-28)

Hii ndio tafsiri ya Tawhiyd. Maneno Yake:

إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ

“Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]… ”

ni sawa na maneno yetu “Hapana mungu wa haki” na maneno yake:

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي

“… [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumba… ”

ni sawa na maneno yetu “isipokuwa Allaah”. Haya yanamaanisha kwamba tafsiri ya Tawhiyd ni kujitenga mbali na vile vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah na kuvitupilia mbali na kuvikemea na kumuabudu Allaah peke yake kwa kumtekelezea aina zote za ´ibaadah.

3-

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ

”Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]! [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumba, basi hakika Yeye ataniongoa.”

Hii ndio tafsiri ya Tawhiyd. Maneno Yake:

إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ

“Hakika mimi najitoa dhima na yale yote mnayoyaabudu [ya batili]!”

ni sawa na sisi kusema “hapana mungu” ilihali:

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي

“… [Simwabudu mwengine yeyote] isipokuwa Yule ameniumba… ”

ni sawa na sisi kusema “isipokuwa Allaah”. Haya yanabainisha ya kwamba maana ya Tawhiyd ni kujitenga mbali na vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah na kuvitupilia mbali na kuvikemea na badala yake mtu ampwekeshe Allaah kwa aina zote za ´ibaadah.

3-

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ

”Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni waungu badala ya Allaah.” (09:31)

Amebainisha kwamba huku pia ni kumshirikisha Allaah na kwamba Tawhiyd ni kutomuabudu mwengine asiyekuwa Allaah pekee na si watawa, marabi, Mitume wala waja wema. Hayo ni tofauti na yale yaliyofanywa na mayahudi na ambao waliwafanya marabi na manaswara ambao wamewafanya watawa kuwa ni waungu badala ya Allaah kwa njia ya kwamba wamewahalalishia yale ambayo Allaah ameharamisha na wakaharamisha yale ambayo Allaah amehalalisha pasi na dalili ijapokuwa yatakuwa ni yenye kwenda kinyume na Sharii´ah ya Allaah na yale waliyokuja nayo Mitume. Kwa hivyo ndipo wakawa ni wenye kuwaabudu kwa vile wamewatii kwa yale yanayopingana na Shari´ah na wakayatanguliza. ´Addiy bin Haatim ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huku ndio kuwaabudu.”[1]

Mwenye kufanya hivo anakuwa mshirikina. Allaah amesema baada ya hapo:

سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُون

“Ametakasika na ametukuka  kutokamana na yale yote wanayomshirikisha.” (49:31)

Faida

Waabudu makaburi wameyafanya makaburi kuwa ni waungu badala ya Allaah. Kwa hiyo ni wajibu kuwabainishia haki. Kwa sababu kitendo chao ni aina kubwa ya ukafiri. Hata hivyo wasiuawe. Inatakiwa kwanza kuwabainishia haki na kuwasimamishia hoja. Endapo wataendelea basi hapo ndipo wanatakiwa kuuawa ikiwa kuna yeyote ambaye anaweza kuwasimamishia adhabu hiyo.

4-

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ

”Wapo katika watu ambao wanafanya badala ya Allaah washirika [na] wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.” (52:165)

Aayah hii pia inafasiri Tawhiyd kwa kuelezea kinyume chake. Wale wanaojifanyia waungu wanawapenda, kuwaadhimisha, wanawaomba, wanawataka msaada na wanawapenda mapenzi maalum ambayo yanapelekea kuwaabudu badala ya Allaah. Hii ni shirki kubwa. Allaah amewasema vibaya watu hawa na akawatishia Moto kama alivosema mwishoni mwa Aayah:

كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ

“Hivyo ndivo Allaah atakavyowaonyesha matendo yao kuwa ni majuto juu yao. Wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.” (02:167)

5- Imepokelewa Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Atakayesema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah, basi imeharamika mali na damu yake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jall).”

Ameipokea Muslim kupitia kwa Sa´d bin Twaariq al-Ashjaa´iy.

Katika upokezi mwingine imekuja: “Atakayesema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na upokezi mwingine imekuja: “Yule ambaye atampwekesha Allaah”. Haya yanabainisha maana ya shahaadah na kwamba maana yake ni kuwa ´ibaadah anatakiwa kufanyiwa Allaah pekee.

Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “… na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah” ni kwamba amekanusha vile vyote vyenye kuabudiwa badala ya Allaah na akaamini hivo moyoni mwake.

Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “… basi imeharamika mali na damu… ” maana yake ni kwamba amekuwa muislamu na hivyo amelazimika kutekeleza Shari´ah za Allaah.

Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “… na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jall)” ni kwamba akiwa ni mkweli ataingia Peponi na kama amesema kwa ulimi wake tu, na si kutoka kwenye moyo wake, anakuwa ni katika wanafiki. Hukumu yake ni kama hukumu ya wanawake duniani na Aakhirah ataingia Motoni.

[1] at-Twabaraaniy(218) na al-Bayhaqiy (20137). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilaat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (3293).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 34-37
  • Imechapishwa: 22/06/2018