06 – Sharti ya sita ya shaahadah – Ikhlaasw

Sharti ya sita ni Ikhaasw. Maana yake ni kuyatakasa matendo kwa kuwa na nia nzuri kutokana na uchafu wote wa shirki. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Zindukeni! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.”[1]

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini.”[2]

قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ

“Sema: “Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.”[3]

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا

”… isipokuwa wale waliotubu, na wakatengeneza, na wakashikamana na Allaah, na wakatakasa dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na waumini. Na Allaah atawapa waumini ujira mkubwa.”[4]

Imethibiti kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye furaha zaidi na uombezi wangu ni yule mwenye kusema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” hali ya kuwa ni mtakasifu kutoka ndani ya moyo wake”.”[5]

Vilevile imesihi kupokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameuharamisha Moto kwa yule mwenye kusema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na huku akitafuta kwa jambo hilo uso na thawabu za Allaah (´Azza wa Jall)”.”[6]

[1] 39:3

[2] 98:5

[3] 39:11

[4] 4:145-146

[5] al-Bukhaariy (1/36).

[6] al-Bukhaariy (1/116).

  • Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/337-338)
  • Imechapishwa: 27/01/2025