Swali: Kwa mfano mchana wa jumatatu nikanuia kulipa deni la alkhamisi na ijumaa inayokuja, nalazimika kila usiku wa siku hizi kunuia mara nyingine? Je, nitalipwa thawabu endapo nitasahau kunuia?

Jibu: Wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wanaona kuwa ni lazima kulala na nia ikiwa swawm ni ya wajibu. Kila funga ambayo ni ya lazima, kama vile Ramadhaan, swawm ya kulipa deni la Ramadhaan au swawm ya nadhiri, basi ni lazima kuilaza nia usiku. Kwa msemo mwingine unatakiwa kunuia usiku kuwa utafunga. Mchana wa jumatatu ukinuia kulipa deni lako la alkhamisi na ijumaa inayokuja na hukutanguliwa kufanya kitu ambacho kinavunja nia hiyo, basi nataraji kuwa kitendo hicho kinafaa. Ni sahihi kwamba unalazimika kulaza nia kila usiku juu ya funga ya wajibu. Hata hivyo nia mahali pake ni moyoni. Kama mtu atanuia kufunga wakati wa mchana na nia ikaendelea kuwepo na isiondoshwe, nataraji kuwa hakuna neno. Kwa sababu anajua ndani ya moyo wake kuwa atafunga kesho na hakuna kikwazo kilichojitokeza. Muda wa kuwa nia yake iliotangulia itakuwepo mpaka jioni, basi itamfanya ni kana kwamba alinuia wakati wa usiku, jambo ambalo halina kizuizi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 19/03/2022