44 – ´Abdul-Wahhaab bin Najdah ametukhabarisha: Baqiyyah ametukhabarisha: az-Zubaydiy ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yaziyd, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, ambaye amesema:
“Bwana mmoja alimwendea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na akasema: “Ee Mtume wa Allaah, ni watu gani bora?” Akasema: “Muumini katika bonde la mlima ambaye anamcha Allaah na kuwasalimisha watu kutokana na shari yake.”[1]
45 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Umm Mubashshir, ambaye amemuuliza Mtume wa Allaah:
“Ni watu gani bora katika daraja?”
Akatoa jawabu kama hilo.
46 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, ambaye amesema:
“Nilimsikia Twaawuus akimuuliza baba yangu juu ya Hadiyth na nikamuona kana kwamba anafunga vidole vyake. Baba yangu akamwambia: “Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Luqmaan alimwambia mwanawe: “Kunyamaza ni hekima na ni wachache wanalitekeleza.” Kisha Twaawuus akamwambia: “Ee Abu Najiyh! Mwenye kusema na kumcha Allaah ni bora kuliko aliyenyamaza na kumcha Allaah.”
47 – Abu Muusa ametukhabarisha: ´Abdus-Salaam bin Haashim al-´Adawiy Abu ´Uthmaan ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid bin Bard al-´Ijliy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuzuia ghadhabu yake basi Allaah anamzuilia adhabu yake. Mwenye kuuchunga ulimi wake basi Allaah anaficha aibu yake. Mwenye kujitolea udhuru mbele ya Allaah basi Allaah anamkubalia udhuru wake.”[2]
48 – Abur-Rabiy´ ametukhabarisha: Muhammad bin Khaazim ametukhabarisha: al-´Awwaam bin Juwayriyah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:
“Mambo manne ni bora: Kunyamaza, ambayo ndio ´ibaadah ya kwanza, kujishusha, kumtaja Allaah na uhaba.”
49 – Ibn Numayr ametukhabarisha: Ibn Abiy ´Ubaydah ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Shimr, ambaye ameeleza kuwa Sa´iyd amesema:
“Kuna mlango wa chuma kati yangu na watu. Siwazungumzishi nao hawanizungumzishi.”
50 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Mis´ar amesema: ´Awn amesema:
“Mtu anapokuwa mgonjwa, anajuta. Anapopata nafuu, anapewa amani. Anapokuwa tajiri, anajaribiwa. Anapokuwa maskini, anahuzunika.”
51 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Watu wa Shaam wametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Khaalid bin Ma´daan, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, ambaye amesema:
“Hali ya chini kabisa ya muumini ni kuwa amwesimama, hali bora ya muovu ni kuwa amelala.”
Sufyaan amesema:
“Anayesema na akashinda ni bora kuliko aliyekaa kimya.”
[1] al-Bukhaariy (6494) na Muslim (1888).
[2] Abu Ya´laa (4338). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (2360).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 13-15
- Imechapishwa: 25/06/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 13-15
Imechapishwa: 25/06/2025
https://firqatunnajia.com/06-ni-watu-gani-bora/