5 – Kuhuisha Bid´ah ya maulidi ni jambo linalofungua mlango wa Bid´ah nyinginezo na kujishughulisha nazo badala ya Sunnah. Kwa ajili hii ndio maana utaona watu wa Bid´ah ni wenye bidii kwelikweli ya kuhuisha mambo ya Bid´ah na wakati huohuo wamezembea katika Sunnah. Sivyo tu bali wanaichukia na kuwafanyia uadui Ahl-us-Sunnah. Kiasi cha kwamba dini yao yote sasa imekuwa ni kuhuisha kumbukumbu za kizushi yakiwemo maulidi. Wamegawanyika mapote mbalimbali ambapo kila pote limehuisha maulidi ya viongozi wao; mfano wa mazazi hayo ni mazazi ya al-Badawiy, Ibn ´Arabiy, ad-Dasuukiy na ash-Shaadhiliy. Mazazi haya hayaishi isipokuwa kunakuja mengine wanayojishughulisha nayo. Hilo limeleta natija ya kuvuka mipaka kwa wafu hawa na wengineo ambapo wanawaomba badala ya Allaah na kuamini kuwa wananufaisha na wanadhuru. Kitendo hichi kimefanya kuwatoa katika Uislamu na kurudi katika dini za kishirikina ambazo Allaah amesema juu yake:
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ
“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”[1]
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ
“Na wale wanaowafanya wengine badala Yake kuwa walinzi [wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.[2]
[1] 10:18
[2] 39:03
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 151
- Imechapishwa: 06/09/2025
5 – Kuhuisha Bid´ah ya maulidi ni jambo linalofungua mlango wa Bid´ah nyinginezo na kujishughulisha nazo badala ya Sunnah. Kwa ajili hii ndio maana utaona watu wa Bid´ah ni wenye bidii kwelikweli ya kuhuisha mambo ya Bid´ah na wakati huohuo wamezembea katika Sunnah. Sivyo tu bali wanaichukia na kuwafanyia uadui Ahl-us-Sunnah. Kiasi cha kwamba dini yao yote sasa imekuwa ni kuhuisha kumbukumbu za kizushi yakiwemo maulidi. Wamegawanyika mapote mbalimbali ambapo kila pote limehuisha maulidi ya viongozi wao; mfano wa mazazi hayo ni mazazi ya al-Badawiy, Ibn ´Arabiy, ad-Dasuukiy na ash-Shaadhiliy. Mazazi haya hayaishi isipokuwa kunakuja mengine wanayojishughulisha nayo. Hilo limeleta natija ya kuvuka mipaka kwa wafu hawa na wengineo ambapo wanawaomba badala ya Allaah na kuamini kuwa wananufaisha na wanadhuru. Kitendo hichi kimefanya kuwatoa katika Uislamu na kurudi katika dini za kishirikina ambazo Allaah amesema juu yake:
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ
“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”[1]
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ
“Na wale wanaowafanya wengine badala Yake kuwa walinzi [wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.[2]
[1] 10:18
[2] 39:03
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 151
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/06-maulidi-yanafungua-mlango-wa-bidah-nyenginezo/