06 – Kutumia wakati. Binti wa Kiislamu! Pupia – Allaah akubariki – kutumia muda wako vyema katika yale yanayokunufaisha katika dunia na Aakhirah yako. Tambua ya kwamba uhai – vovote utavyokuwa mrefu – ni mfupi. Wakati wa mwanamke wa Kiislamu ni mupi sana. Isiweje hivo ilihali wakati wake ndio maisha yake na mtaji wake? Akiuchunga, basi atafaulu na kushinda, na akiupoteza, basi atakula khasara na kuangamia.
Allaah (´Azza wa Jall) ameuapia muda maeneo mengi ndani ya Kitabu Chake ili kuonyesha umuhimu wake. Amesema (Ta´ala):
وَالْفَجْرِ
”Naapa kwa alfajiri!”[1]
وَالضُّحَىٰ
”Naapa kwa dhuhaa.”[2]
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ
”Naapa kwa usiku unapofunika.”[3]
Kwa hivyo inampasa mwanamke wa Kiislamu amche Allaah juu ya nafsi yake na auchunge muda wake kwa yale yanayomnufaisha. Mwanamke anatakiwa asiache muda wake kupotea bure isipokuwa iwe kwa jambo linalomnufaisha. Ajihesabu nafsi usiku na mchana, asubuhi na jioni, katika maneno, matendo yake, yale anayoyaacha, katika maneno yake, masikio na macho yake. Lengo ni ili apate faida kwa muda wake na dini yakeisalimike na imani yake itakasike. Mshairi amesema:
Wakati ndio kitu cha thamani zaidi ninachopaswa kuchunga
nakuona mwenzangu ndio kitu rahisi zaiidi kukipoteza!
Kwa hivyo ni lazima kwa mwanamke wa Kiislamu atumie vyema fursa ya uhai, ujana, afya na wakati huru wa kufanya matendo mema maadamu anazo nguvu, muweza, mzima wa mwili, mwenye kusikia na mwenye kuona. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya mambo manne: umri wake aliuteketeza katika mambo gani, ujana wake aliuteketeza katika mambo gani, mali yake aliipata kivipi na akaitumia wapi na mwili wake aliutumia vipi na elimu yake aliifanyia nini?”[4]
“Faidika na mambo matano kabla ya mambo matano: ujana wako kabla ya uzee wako, afya yako kabla ya ugonjwa wako, uhai wako kabla ya kifo chako, muda wako huru kabla ya kushughulishwa kwako na utajiri wako kabla ya umaskini wako.”[5]
[1] 89:1-2
[2] 93:01
[3] 92:01
[4] al-Haakim na al-Bayhaqiy katika ”Shu´ayb-ul-Iymaan”. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (01/243) nr. 1077.
[5] at-Tirmidhiy ambaye amesema ni nzuri na Swahiyh. al-Mundhiriy amesema:
”Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.” (at-Targhiyb at-Tarhiyb (04/316)).
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 14-16
- Imechapishwa: 09/02/2026

Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 14-16
Imechapishwa: 09/02/2026
https://firqatunnajia.com/06-kutumia-wakati-vizuri/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket