06. Kuomba msamaha baada ya kutenda dhambi

27 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake, lau msingelikuwa mnafanya dhambi basi Allaah angekuondosheni na akaleta watu wengine wanaotenda dhambi na kumuomba Allaah msamaha ambapo akawasamehe.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameapa – naye ni mkweli ingawa asingeapa – lakini amefanya hivo ili kutilia mkazo jambo hili. Mara nyingi alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiapa kwa Ambaye nafsi yake imo mkononi Mwake. Hadiyth inafahamisha kuwa Allaah yuko na mkono na wanaraddiwa waliopinga mkono huo. Inafahamisha kuwa nafsi zimo mkononi mwa Allaah. Aidha Hadiyth inafahamisha kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewakadiria viumbe kutenda dhambi kutokana na ile hekima ambayo Allaah anaijua ya mja kurejea Kwake, kutubia Kwake kutokana na madhambi, kutambua uola wa Allaah na kukiri dhambi aliyofanya.

[1] Muslim (2749).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 06/10/2025