3 – Vitabu Vyake.
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini Vitabu vyote vya Allaah alivyoteremsha kwa Mitume. Wanaamini vile walivyovijua kama Tawraat, Injiyl, Zabuur na Qur-aan. Vilevile wanaamini vile wasivyovijua kwa njia ya ujumla. Amesema (Ta´ala):
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ
“Kwa hakika Tuliwatuma Mitume Wetu kwa hoja bayana na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na mizani.” (57:25)
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini ya kuwa Allaah ameteremsha Vitabu kwa Mitume na kwamba ni haki. Wanaamini vilevile kuwa Vitabu hivyo ni katika maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Miongoni mwa Vitabu hivyo ni pamoja vilevile na Tawraat, Injiyl, Zabuur na Qur-aan. Hivi ni miongoni mwa Vitabu alivyoteremsha.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 13
- Imechapishwa: 16/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket