12 – ´Aliy bin ´Abdil-Wahhaab as-Sukkariy amenikhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas al-Kharraaz ametukhabarisha: Ja´far bin Ahmad al-Marwaziy ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Muhammad bin Ismaa´iyl ametukhabarisha: Ibn Fudhwayl ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym al-Hajriy, kutoka kwa Abu ´Iyaadh, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:
”Elimu isiyofanyiwa kazi ni kama mfano wa limbikizo isiyotolewa kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
13 – Abul-Husayn Muhammad bin al-Husayn bin Muhammad bin al-Fadhwl al-Qattwaan ametukhabarisha: Abu Muhammad ´Abdullaah bin Ja´far bin Darstuuyah an-Nahwiy ametukhabarisha: Ya´quub bin Sufyaan ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym ametuhadithia: al-Waliyd ametuhadithia: al-Qaasim bin Hazzaan ametuhadithia: Nimemsikia az-Zuhriy akisema:
”Watu hawaamini matendo ya mtendaji asiyejua. Wala hawaridhii maoni ya mwanachuoni asiyefanya vitendo.”[2]
14 – Muhammad bin Ahmad bin Rizquuyah ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametukhabarisha: Hanbal bin Ishaaq ametuhadithia: Sulaymaan bin Ahmad al-Waasitwiy ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha: al-Qaasim bin Hazzaan amenihadithia kuwa amemsikia az-Zuhriy akisema:
”Watu hawaridhii maoni ya mwanachuoni asiyefanya vitendo na wala maoni ya mtendaji asiyejua.”
15 – al-Qaadhwiy Abul-´Alaa’ Muhammad bin ´Aliy bin Ahmad bin Ya´quub al-Waasitwiy ametukhabarisha: ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Barniy ametuhadithia huko Waasitw: Yahyaa bin Swaa´id ametuhadithia: Muhammad bin Abiy ´Abdir-Rahmaan al-Muqriy ametuhadithia: Hakkaam bin Sulm ar-Raaziy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Sinaan, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa ´Aliy bin al-Husayn, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Matendo na imani ni vitu viliwi vinavyoenda sambamba. Kimoja hakifanyi kazi hadi kiwe na mwenzake.”[3]
Yahyaa amesema: ”Abu Yahyaa Muhammad bin Abiy ´Abdir-Rahmaan amesema:
”Zaidi ya miaka khamsini iliyopita baba yangu alikuja pamoja nami kuyasikia haya kutoka kwa Hakkaam.”
16 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametukhabarisha: Husayn bin Abiy Ma´shar ametuhadithia: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, kutoka kwa Furaat bin Salmaan, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:
”Hutokuwa mwanachuoni mpaka uwe mwenye kuelimika. Na hutokuwa mwenye kuelimika mpaka uyafanyie kazi yale uliyojifunza.”[4]
[1] Cheni ya wapokezi haina neno. Imepokelewa pia kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth ameipokea Imaam Ahmad.
[2] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri na yenye kukatika. Vivyo hivyo kuhusu cheni inayofuatia. Ibn Abiy Haatim amesimulia kuwa baba yake amesema kuhusu al-Qaasim bin Hazzaan:
”Shaykh anayeaminika.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (3/2/123))
[3] Dhaifu kwa sababu ya Swahabah aliyekosekana kwenye cheni ya wapokezi. Isitoshe simjui ni nani huyu Muhammad bin Abiy ´Abdir-Rahmaan al-Muqriy. Abu Sinaan jina lake ni Sa´iyd bin Sinaan al-Barjamiy ambaye alikuwa mwenye kuaminika, mwenye kukosea.
[4] Dhaifu kwa sababu ya kukatika baina ya Furaat bin Salmaan na Abud-Dardaa’.
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 24-26
- Imechapishwa: 07/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)