06. Hadiyth ”Hakika tulimuona Mtume wa Allaah akiswali ndani ya viatu”

Ibn Maajah amesema: ´Aliy bin Muhammad ametuhadithia: Yahyaa bin Aadam ametuhadithia: Zuhayr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:

”Hakika tulimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali ndani ya viatu na soksi za ngozi.”[1]

Hadiyth imepokelewa pia na Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1/84), Ibn Abiy Shaybah (2/416), Ahmad (1/461) na at-Twahaawiy (1/511). Baadhi wametamka wazi kwamba Abu Ishaaq hakumsikia ´Alqamah. al-Buuswayriy amesema:

“Katika cheni ya wapokezi yumo Abu Ishaaq as-Sabiy´iy ambaye alichanganyikiwa mwishoni mwa maisha yake. Kwa mujibu wa Abu Zur´ah alipokea kutoka kwa Zuhayr bin Mu´aawiyah bin Khadiyj ambaye alichanganyikiwa mwishoni mwa maisha yake.”[2]

Hadiyth kwa cheni ya wapokezi hii ni dhaifu, lakini ni sawa kuitumia kwa lengo la kutilia nguvu.

[1] Ibn Maajah (1/330). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (858).

[2] Miswbaah-uz-Zujjaah, uk. 125.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 9-10
  • Imechapishwa: 28/05/2025