45 – Abu Maalik al-Ashja´iy amesimulia kutoka kwa baba yake: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimfunza anayesilimu aseme:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي وَارْزُقْنِي

“Ee Allaah! Nisamehe, nirehemu, niongoze na uniruzuku.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Alikuwa mtu anaposilimu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamfunza swalah, kisha anamwamrisha aombe maneno yafuatayo:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وَارْحَمْنِي، وَاهْدِنِي، وَعَافِنِي وَارْزُقْنِي

“ Ee Allaah! Nisamehe, nirehemu, niongoze, nisalimishe na uniruzuku.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kujiliwa na mtu aliyemuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Niseme nini wakati ninapomuomba Mola wangu?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Sema:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي، وَعَافِنِي، وَارْزُقْنِي

“Ee Allaah! Nisamehe, nirehemu, nisalimishe na uniruzuku.”

na akikusanya vidole vyake isipokuwa kidole gumba. Hakika mambo haya [manne] yanakukusanyia dunia na Aakhirah yako.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii inajulisha fadhilah ya du´aa hii na kwamba inakukusanyia dunia na Aakhirah. Imepokelewa katika “as-Sunan” ya kwamba imesuniwa kuiomba kati ya Sujuud mbili[2].

[1] Muslim (2697).

[2] Sunan ya Abu Daawuud (850).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 51
  • Imechapishwa: 13/10/2025