06. Anayoruhusiwa kufanya anayetaka kuchinja Udhhiyah

Hapana vibaya kwa mwanamume au mwanamke kuosha kichwa katika siku hizi kumi, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kukata, si kuosha. Pia Muhrim ameruhusiwa kuosha kichwa chake.

Anayetaka kuchinja Udhhiyah kisha akawa na azma ya kwenda kuhiji, basi asikate nywele wala kucha zake anapoingia ndani ya Ihraam, kwani hiyo ni Sunnah pale panapohitajika, hivyo upande wa kuacha unakuwa na nguvu zaidi. Lakini ikiwa ni mwenye kufanya hijjah ya Tamattu´, basi atapunguza nywele zake baada ya kukamilisha ´Umrah yake. Kwa sababu hiyo ni sehemu ya ´ibaadah kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi. Vilevile atapunguza nywele zake baada ya kupiga vijiwe kwenye kiguzo cha ´Aqabah siku ya ´Iyd.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 9
  • Imechapishwa: 05/05/2025