05. Yule anayetaka kuwa tajiri na kuishi maisha marefu

14 – Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia: al-Layth ametuhadithia, kutoka kwa ´Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, ambaye amenikhabarisha kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule anayetaka kukunjuliwa riziki yake na kuishi maisha marefu, basi awaunge ndugu zake.”

15 – Muhammad bin Sa´iyd al-Khuzaa´iy ametuhadithia: Hazm bin Abiy Hazm al-Qutwa´iy ametuhadithia: Nimemsikia Maymuun bin Siyaah: Nimemsikia Anas: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anayetaka kuishi maisha na kuzidishiwa riziki yake, basi awatendee wema wazazi wake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 16/12/2024