05. Watetee Uislamu dhidi ya mashambulizi

Watu wote wenye busara wanaona ile haja kubwa ya Ummah katika kila wakati na khaswa katika wakati wa sasa ya kuwa na walinganizi wema na wenye kutengeneza, washauri na wenye huruma. Vita vya kifikra vimeshambulia fikira, ´Aqiydah na maadili mema ya Ummah huu kwa njia ya fitina ya matamanio na utata katikati yake. Ni kama alivosema mshairi:

Vilele vya shari vimejitokeza

ilihali kheri ikipigwa mishale

Dini inasambaratishwa kandokando na dhaifu

na haki inahitaji mwenye kuinusuru, imeachwa kama ilivyojaaliwa

Upuuzi wa kila tarishi na mwendawazimu

unazishambulia nyoyo na kupasua vichwa

Wanafugnua mimbari za udanganyifu hadharani

ili pande zote nne ziweze kutetemeka

Kwa ajili hiyo waislamu – na khaswa wanazuoni na wanafunzi – wanatakiwa kukabiliana na shari hizi na kuzitokomeza kila mmoja awezavyo. Allaah hapotezi ujira wa wafanyao wema. Wakifanya hivo, basi wataokoka wao na jamii nzima. Na wakiacha kufanya hivo, basi wote wapata dhambi. Majaribio na majanga yatatokea kwa kiasi cha mapungufu yao.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 9
  • Imechapishwa: 29/07/2022