21 – Inatakiwa kuamini uombezi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watenda madhambi na waliokosea siku ya Qiyaamah na katika Njia. Atawatoa kutoka kwenye kina cha Moto. Hakuna Mtume isipokuwa ana uombezi na kadhalika wakweli, mashahidi na waja wema. Baada ya hapo Allaah ataonyesha fadhilah nyingi kwa yule anayemtaka na baada ya kuwa wameunguzwa na wamekuwa makaa, watatoka Motoni.

22 – Inatakiwa kuamini Njia ilioko juu ya Moto. Njia itamkaba yule Allaah anamtaka,  itamwacha yule Allaah anamtaka na ataanguka ndani ya Moto yule Allaah anamtaka. Watakuwa na mwanga kutegemea na imani zao.

23 – Inatakiwa kuamini Mitume na Malaika.

24 – Inatakiwa kuamini kuwa Pepo na Moto vyote ni haki. Vyote viwili vimeumbwa. Pepo iko kwenye mbingu ya saba na paa lake ni ´Arshi, ilihali Moto uko chini kabisa ya ardhi ya saba. Vyote viwili vimeshaumbwa. Allaah (Ta´ala) alijua idadi ya watu wa Peponi na ni nani atayeingia na idadi ya watu wa Motoni na wataouingia. Vitu viwili hivyo havitotoweka kamwe na vitabaki kwa kubakia kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) kwa muda wa kudumu milele na milele.

25 – Aadam (´alayhis-Salaam) alikuwa katika Pepo ya milele, iliyoumbwa. Baada ya hapo akatolewa baada ya kumuasi Allaah (´Azza wa Jall).

26 –  Inatakiwa kuamini al-Masiyh ad-Dajjaal.

27 – Inatakiwa kuamini kuwa ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) atateremka. Atashuka na kumuua ad-Dajjaal. Ataoa na kuswali nyuma ya imamu kutoka katika kizazi cha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Atakufa na waislamu watamzika.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 16/12/2024