05. Upunguani wa Qadariyyah juu ya uelewa wa uola

Watu wa maoni ya pili kadhalika wanaraddiwa na dalili na ukweli wa mambo. Dalili zinabainisha wazi kuwa utashi wa mja unafuata utashi wa Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“[Kitabu] hichi si jengine isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu – Kwa yule anayetaka katika nyinyi anyooke. Lakini hamtotaka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ

“Mola wako anaumba na kuchagua Atakavyo.”[2]

وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Allaah anaita kwendea katika nyumba ya amani na anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.”[3]

Wale walio na madhehebu haya uhakika wa mambo ni kwamba wanakataa moja ya kipengele cha uola. Wanadai kuwa katika milki ya Allaah kunapitika asiyoyataka na kuyaumba. Kila kilichopo kipo kwa kuwa Allaah (Ta´ala) ametaka kiwepo. Yeye ndiye muumba wa kila kitu na ndiye mwenye kukadiria kila kitu. Vilevile wanaenda kinyume na yale mambo yanayojulikana fika ya kwamba viumbe wote ni milki ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hiyo kila kitu ni milki ya Allaah (´Azza wa Jall). Ni jambo lisilowezekana kukawa katika milki ya Allaah asichokitaka (Tabaarak wa Ta´ala) kiwepo.

[1] 81:27-29

[2] 28:68

[3] 10:25

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/219-220)
  • Imechapishwa: 25/10/2016