3 – Baleghe. Si wajibu kwa mtoto mdogo kufunga. Hata hivyo ikiwa mtoto anaweza kufunga, swawm yake ni sahihi na anaamrishwa kufanya hivyo kwa lengo la mazoezi, kama anavyoamrishwa kuswali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na umri wa miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na umri wa miaka kumi na watenganishe vitandani.”[1]
Salaf katika Maswahabah wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiwazoweza watoto wao wa kiume na wa kike kufunga wakiweza kufanya hivo. Iwapo mmoja wao analia kwa njaa, walimpa kitu cha kuchezea kimpunguzie njaa mpaka ufike wakati wa kufungua swawm. ar-Rabiy´ bint Mu´aadh ameeleza:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma ujumbe kwa vijiji vya Answaar siku ya ´Aashuuraa´: Aliyeamka akiwa amefungua, basi akamilishe sehemu ya mchana wake iliyobakia, na aliyeamka akiwa amefunga, basi na aendelee kufunga.” Tulikuwa tunafunga baada ya hapo na tukawafundisha watoto wetu kufunga. Tukiwapa vipande vya kuchezea vilivyotengenezwa kwa sufi. Mmoja wao anapolia kwa njaa, tunampa mpaka wakati wa kufuturu.”[2]
Kuhusu ni lini swawm ilifaradhishwa, Allaah (Ta´ala) aliifaradhisha kufunga Ramadhaan mwaka wa pili baada ya kuhajiri[3]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafunga Ramadhaan tisa. Aliishi Madiynah miaka kumi.
[1] Ahmad (6689), Abu Daawuud (395) na al-Haakim (708). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (1/266).
[2] al-Bukhaariy (1960) na Muslim (1136).
[3] al-Majmuu´ Sharh-ul-Mu´addhab (01/178) na ”al-Umdah fiy Sharh-il-´Aqiydah” (02/839) ya Ibn ´Attwaar.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/433-434)
- Imechapishwa: 16/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)