4 – Kusherehekea ukumbusho wa mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mbali na kwamba ni Bid´ah na ni kujifananisha na wakristo – na yote hayo mawili ni haramu – ukiongezea juu ya hayo vilevile ni njia inayopelekea katika kuvuka mipaka na kupitiliza mipaka katika kumuadhimisha kwa kiasi cha kwamba anafikia mpaka kuombwa na kumtaka uokozi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) badala ya Allaah. Huo ndio uhakika wa mambo yanayofanywa na wale wenye kusherehekea Bid´ah ya maulidi ambapo wanamuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) badala ya Allaah, kumtaka msaada na kuimba mashairi ya shirki wakati wa kumsifu. Moja katika mashairi hayo ni ”al-Burdah” na nyinginezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kupitiliza mipaka katika kumsifu pindi aliposema:
“Msinifu kwa kupitiliza kama walivyopindukia wakristo kwa ´Iysaa bin Maryam. Hakika mimi ni mja. Hivyo semeni “Mja wa Allaah na Mtume Wake.”[1]
Maana yake ni kwamba msivuke mipaka katika kunisifu na kunitukuza kama walivofanya wakristo katika kumsifu na kumtukuza ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka wakafikia kumuabudu yeye badala ya Allaah. Isitoshe Allaah amewakataza hilo pale aliposema:
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ
“Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Allaah isipokuwa ukweli. Hakika hapana vyengine al-Masiyh‘ Iysaa mwana wa Maryam ni Mtume wa Allaah na ni neno Lake [la kuwa!] alompelekea Maryam na Roho [aloumba kwa amrisho] kutoka Kwake.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametukataza na kuvuka mipaka kwa kuchelea tusije kufikwa na yaliyowafika wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tahadharini na kuvuka mipaka! Hakika kilichowafanya kuangamia waliokuwa kabla yenu ilikuwa ni kuvuka mipaka.”[3]
[1] al-Bukhaariy (3445).
[2] 04:171
[3] an-Nasaa’iy (05/268). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan-in-Nasaa’iy” (2863).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 150-151
- Imechapishwa: 06/09/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 150-151
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/05-ndani-ya-maulidi-kuna-kuchupa-mipaka/