11 – Ahmad bin Muhammad bin ´Umar ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Ibraahiym bin Abiyl-Layth ametuhadithia: Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa Ya´quub bin ´Utbah bin al-Mughiyrah bin al-Akhnas, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma mashairi ya Umayyah bin Abiys-Swalt:
Bwana mmoja na fahali chini ya mguu wake wa kuume
tai chini ya mwingine wa pili na simba mwenye kulinda
Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Amesema kweli, amesema kweli.” Kisha akasoma:
Jua linachomoza mwishoni mwa kila usiku jekundu
ambapo inakuwa na rangi ya waridi
Haituchomozei katika mzunguko wake
isipokuwa linaadhibiwa au kuchapwa viboko
Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Umesema kweli.”
Hadiyth hii ni yenye kutambulika kutoka kwa Muhammad bin Sulaymaan. Ameipokea ´Abdah bin Sulaymaan, Yuunus bin Bukayr na wengineo.
12 – Ahmad bin Sulaymaan bin Hadhlam ametukhabarisha: Abu Zur´ah ametuhadithia: Yusuuf bin Bahluul ametuhadithia: ´Abdah bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa Ya´quub bin ´Utbah, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) alimsadikisha Umayyah bin Abiys-Swalt katika mashairi yake pale aliposema:

13 – ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdillaah al-Bajaliy ametukhabarisha: Yaziyd bin Muhammad bin ´Abdis-Swamad ametuhadithia: Abun-Nadhwr Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Yaziyd bin Rabiy´ah ametuhadithia: Abul-Ash´ath as-Swan´aaniy ametuhadithia: Nimemsikia Thawbaan akisimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”al-Jabbaar atasogea mbele, aweke mguu Wake juu ya Daraja na kusema: ”Naapa kwa ufalme na utukufu Wangu! Leo hakuna dhuluma yoyote itayonipia.” Atawafanya viumbe wote kutendeana haki kati yao. Kiasi cha kwamba atamfanya mnyama asiye na pembe alipe kisasi kutoka kwa mnyama mwenye pembe aliyempiga.”
14 – Ahmad bin Sulaymaan bin Hadhlam ametukhabarisha: Abu Zur´ah ametuhadithia: Abu Swaalih ametuhadithia: Mu´aawiyah bin Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa Raashid bin Sa´d, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Allaah (´Azza wa Jall) atafuta dhuluma zote siku ya ijumaa ambapo ataziweka chini ya unyayo Wake. Isipokuwa tu mshahara wa mfanyakazi, uchinjaji wa wanyama wa kufugwa na bikira iliyopotea.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 43-44
- Imechapishwa: 09/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 43-44
Imechapishwa: 09/06/2026
https://firqatunnajia.com/05-masimulizi-mengine-yanayotilia-nguvu-kuhusu-unyayo-wa-allaah/