12 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuna maneno mawili mepesi zaidi kwenye ulimi, mazito zaidi kwenye mizani na ni yenye kupendeza zaidi na Mwingi wa huruma:

سُبْحَانَ اللَّهِ ، وبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللَّهِ الْعَظِيمِ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na sifa zote njema ni Zake. Allaah, hali ya kuwa ametukuka, ametakasika kutokamana na mapungufu.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha fadhilah za maneno haya mawili na pia inafahamisha ubora wa Tasbiyh ambayo ni kumtakasa Allaah kutokana na yale mapungufu yasiyomstahikia. Kwa hivyo ni lazima kwa muislamu kuyapupia na asipuuze dhikr hii.

Hadiyth inathibitisha pia mizani huko Aakhirah na pia inawaraddi wale walioipinga. Ni mizani yenye kuhisiwa yenye masahani mawili.

Hadiyth inamthibitishia Allaah sifa ya kupenda.

Hadiyth inajulisha pia kwamba ni lazima dhikr iwe kwa kutamka kwa mdomo. Haitoshi kufikiria kwa moyo. Lakini ikiwa moyo pamoja na mdomo vitakutana ndio bora zaidi.

[1] al-Bukhaariy (6406) na Muslim (2694).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 20
  • Imechapishwa: 29/09/2025