05. Kusamehewa kwa madhambi makubwa na madogo

26 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema anaposujudu:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ: دِقَّهُ وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، وَعَلاَنِيَّتَهُ وَسِرَّهُ

“Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote; ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za kujificha.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha kusamehewa kwa madhambi, makubwa na madogo, za mwanzo na za mwisho, zinazofanywa kwa dhahiri na zinazofanywa kwa siri.

[1] Muslim (482).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 31
  • Imechapishwa: 06/10/2025