9 – Abu Sa´iyd al-Hasan bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Kaatib ametukhabarisha huko Aswbahaan: al-Qaadhwiy Abu Bakr Muhammad bin ´Umar bin Sulm al-Haafidhw ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Imraan an-Najjaar amenihadithia: Ibraahiym bin Sa´iyd ametuhadithia: al-Hasan bin Bishr ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Thuwayr bin Abiy Faakhitah, kutoka kwa Yahyaa bin Ja´dah, kutoka kwa ´Aliy, aliyesema:

”Enyi wabeba elimu! Ifanyieni kazi! Kwani hakika mwanachuoni ni yule mwenye kufanya matendo. Itafika wakati watakuwepo watu ambao wanabeba elimu na kujifakhari baadhi kwa wengine kiasi cha kwamba, itafikia mtu kumkasirikia jirani yake kwa sababu tu mtu huyo anaketi kwa mwingine. Hao matendo yao hayapandishwi juu mbinguni.”[1]

10 – Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin Ibraahiym bin Ismaa´iyl al-Bazzaaz ametukhabarisha huko Baswrah: Abu ´Aliy al-Hasan bin Muhammad bin ´Uthmaan al-Fasawiy ametuhadithia: Ya´quub bin Sufyaan ametuhadithia: Khalaf bin al-Waliyd Abul-Waliyd ametuhadithia: Khaalid bin ´Abdillaah ametuhadithia…ح Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Yazdaad al-Qaari’ ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ibraahiym bin ´Abdil-Malik al-Aswbahaaniy ametukhabarisha jambo hilo: Muhammad bin ´Aliy bin Makhlad al-Farqadiy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Amr ametuhadithia: Khaalid bin ´Abdillaah ametuhadithia…ح Abu Muhammad Yahyaa bin al-Hasan bin al-Hasan bin ´Aliy bin al-Mundhir al-Qaadhwiy ametukhabarisha: ´Aliy bin ´Umar bin Ahmad al-Haafidhw ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa bin Haaruun al-Iskaafiy ametuhadithia huko Iskaaf: Ishaaq bin Shaahiyn ametuhadithia: Khaalid bin ´Abdillaah ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:

”Jifunzeni, jifunzeni. Na mkishajifunza, basi fanyeni matendo.”[2]

Kwa mujibu wa upokezi wa Ibn-ul-Mundhiriy alisema ”Jifunzeni” mara moja.

11 – Abu Sa´iyd Muhammad bin Muusa bin al-Fadhwl as-Swayrafiy ametukhabarisha huko Naysaabuur: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia: Haaruun bin Sulaymaan al-Aswbahaaniy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan…ح Abu Sa´iyd al-Hasan bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Hasnuuyah al-Aswbahaaniy ametukhabarisha: Abu Ja´far Ahmad bin Ibraahiym bin Yuusuf at-Tamiymiy ametuhadithia: ´Imraan bin ´Abdir-Rahiym ametuhadithia: al-Husayn bin Hafsw ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Tamiym bin Salamah, kutoka kwa Abu ´Ubaydah, aliyesimulia kuwa ´Abdullaah amesema:

”Jifunzeni. Yule aliyejifunza afanyie kazi kwa vitendo.”[3]

Namna hii ndivo ulivo upokezi wa Ibn Mahdiy. Abu Sa´iyd hakututajia Tamiym bin Salamah katika cheni yake ya wapokezi. Ibn Hasnuuyah amesimulia kutoka kwa Abu ´Ubaydah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye amesema:

”Jifunzeni, enyi watu! Yule mwenye kujifunza atendee kazi kwa vitendo.”

[1] Cheni yake ya wapokezi imekatika. Isitoshe Thuwayr bin Abiy Faakhitah alikuwa mnyonge.

[2] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Yaziyd bin Abiy Ziyaad alikuwa akiitwa al-Qurashiy al-Haashimiy.

[3] Cheni yake ya wapokezi imekatika. Abu ´Ubaydah bin ´Abdillaah bin Mas´uud hakusikia kutoka kwa baba yake. Inatosha ile cheni ya wapokezi ilio kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 22-24
  • Imechapishwa: 07/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy