Katika mada hii mahususi mara nyingi hutajwa jinsi Aayah fulani imeteremshwa kuhusiana na jambo fulani, khaswa ikiwa inahusiana na mtu fulani. Miongoni mwa hayo ni ile Aayah inayowakataza wanaume kuwafananisha wake zao na migongo ya mama zao kwamba imeteremshwa juu ya mwanamke wa Aws bin as-Swaamit, kwamba Aayah inayowakataza waume kujilaani ikiwa anasema uwongo imeteremshwa juu ya ´Uwaymir al-´Ajlaaniy au Hilaal bin Umayyah, kwamba Aayah ya ambaye ameacha mirathi na hana jamaa wa kumrithi imeteremshwa juu ya Jaabir bin ´Abdillaah, kwamba Aayah:
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ
“Wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allaah.”[1]
imeteremshwa juu ya Banuu Quraydhwah na Banuun-Nadhwiyr, kwamba Aayah:
وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ
”Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo… ”[2]
imeteremshwa juu ya Badr, kwamba Aayah:
يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ
“Enyi walioamini! Mauti yanapomfikia mmoja wenu wakati anapousia, basi chukueni ushahidi… ”[3]
Imeteremshwa juu ya Tamiyn ad-Daariy na ´Adiy bin Baddaa’ na masimulizi ya Abu Ayyuub kwamba Aayah:
وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ
“Wala msijitupe kwa mikono yenu katika maangamizi.”[4]
”Imeteremshwa juu yetu Wanusuraji.”
Kuna mifano mingi inayofanana na hiyo ya jinsi wanavyotaja jinsi Aayah zilivyoteremshwa juu ya washirikina wa Makkah, mayahudi na manasara katika watu watu wa Kitabu au waumini. Wale waliosema hivo hawamaanishi kuwa hukumu yaza Aayah zinawahusu hao watu binafsi tu na si mwingine yeyote – hakuna muislamu au mtu mwenye akili timamu kabisa anayesema hivyo.
Ingawa watu wanaweza kutofautiana juu ya tamko la jumla linafanywa maalum na sababu yake au hapana, hakuna mwanachuoni yeyote wa Kiislamu anayesema kwamba maandishi ya jumla ya Qur-aan na Sunnah yanahusu tu mtu fulani. Kubwa wanachoweza kusema ni kwamba Aayah hiyo inawahusu watu wa aina hiyo. Kwa hivyo itakusanya ile hali inayofanana na hali ya mtu huyo na bila ujumla wake kuwa kutokana na tamko hilo. Ikiwa Aayah imeteremshwa kuhusiana na tukio fulani na haina maamrisho wala makatazo, inatumika kwa mtu huyo na kwa watu wengine wote walio katika hali kama hiyo. Na ikiwa ina sifa au masimango, basi inatumika pia kwa mtu huyo na kwa watu wengine wote walio katika hali kama hiyo.
[1] 5:49
[2] 8:16
[3] 5:106
[4] 2:195
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 34-37
- Imechapishwa: 23/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)