712- an-Nasaa´iy amepokea mfano wake kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah[1]. Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Amr al-´Aasw imeshatangulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayetawadha na akaoga, akasogea karibu na akaja mapema, akajongea karibu na kusikiliza, basi analipwa kwa kila hatua moja aliyopiga kisimamo cha usiku cha mwaka mzima na swawm yake.”[2]

Vilevile kumeshatangulia Hadiyth mfano wake kutoka kwa Aws bin Aws.

[1] Pamoja na Muslim, Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah, kama nilivyobainisha katika asili.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/445)
  • Imechapishwa: 25/01/2018