44 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى، وَالتُّقَى، وَالْعَفَافَ، وَالْغِنَى
”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba uongofu, uchaji, utakasifu na utajiri.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba uongofu… ”
Bi maana unamuomba Allaah akuongoze katika haki na yaliyo ya sawa na yale maneno na vitendo unavyovipenda na kuviridhia.
Uchaji bi maana unamuomba Allaah akufanye uwe mwenye kumcha na mwenye kufanya matendo mema. Ni kama kwamba uongofu unamuomba Allaah elimu na uchaji unamuomba Allaah matendo mema.
Utakasifu bi maana akuepushe na yasiyokuwa halali. Kwa maana nyingine unamuomba Allaah akuepushe na mambo ya haramu.
Utajiri bi maana akutosheleze na halali kutokamana na haramu na kutosheka kutokana na vilivyomo mikononi mwa watu kwa sababu ya vile vilivyoko kwa Allaah.
Du´aa hii ni miongoni mwa zile zilizokusanya.
[1] Muslim (2721).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 50
- Imechapishwa: 13/10/2025
44 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى، وَالتُّقَى، وَالْعَفَافَ، وَالْغِنَى
”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba uongofu, uchaji, utakasifu na utajiri.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba uongofu… ”
Bi maana unamuomba Allaah akuongoze katika haki na yaliyo ya sawa na yale maneno na vitendo unavyovipenda na kuviridhia.
Uchaji bi maana unamuomba Allaah akufanye uwe mwenye kumcha na mwenye kufanya matendo mema. Ni kama kwamba uongofu unamuomba Allaah elimu na uchaji unamuomba Allaah matendo mema.
Utakasifu bi maana akuepushe na yasiyokuwa halali. Kwa maana nyingine unamuomba Allaah akuepushe na mambo ya haramu.
Utajiri bi maana akutosheleze na halali kutokamana na haramu na kutosheka kutokana na vilivyomo mikononi mwa watu kwa sababu ya vile vilivyoko kwa Allaah.
Du´aa hii ni miongoni mwa zile zilizokusanya.
[1] Muslim (2721).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 50
Imechapishwa: 13/10/2025
https://firqatunnajia.com/05-duaa-ya-uongofu-uchaji-utakasifu-na-utajiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket