Tawhiyd imegawanyika aina mbili:
1 – Tawhiyd katika utambuzi na kuthibitisha, nayo ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Tawhiyd hii inawakilishwa na kukubali Muumba, kupwekeka Kwake juu ya kuumba, kuyaendesha mambo, kuhuisha, kufisha, kuleta kheri na kuzuia shari. Aina hii anakaribia kutokuwepo kiumbe yeyote anayeipinga, wakiwemo washirikina licha ya shirki zao walikuwa wakiikubali. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala) katika maneno Yake:
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ
”Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini au nani anayemiliki kusikia na kuona na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu na anayemtoa mfu kutoka aliye hai na nani anayeendesha mambo?” Watasema: “Ni Allaah”, basi sema: “Je, basi kwa nini hamchi?”[1]
Mfano wa Aayah kama hizi ni nyingi. Ndani yake kuna ubainifu wa wazi ya kwamba washirikina walikuwa wakiikubali aina hii ya Tawhiyd. Walichokuwa wakipinga ni aina ya pili ya Tawhiyd:
2 – Tawhiyd-ul-´Ibaadah. Inawakilishwa na kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika maombi na nia katika kila aina ya ´ibaadah anayofanya mja. Hivyo ndivyo inavofahamisha neno “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Neno hili linamthibitishia Allaah pekee aina zote za ´ibaadah na kumkanushia mwengine asiyekuwa Yeye. Kwa ajili hiyo wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowataka washirikina walitamke walikataa na wakasema:
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ
“Amewafanya waungu kuwa ni mungu Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno!”[2]
Kwa sababu walijua kwamba yule mwenye kulitamka amejikubalisha mwenyewe ubatilifu wa kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah na badala yake kumthibitishia ´ibaadah Allaah pekee. Kwani mungu (الإله) maana yake ni mwabudiwa (المعبود).
[1] 10:31
[2] 38:05
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 09-11
- Imechapishwa: 21/03/2019

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 09-11
Imechapishwa: 21/03/2019
https://firqatunnajia.com/05-aina-mbili-za-tawhiyd/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket