17 – Inatakiwa kuamini Kuonekana siku ya Qiyaamah. Watamuona Allaah (´Azza wa Jall) kwa macho yaliyo vichwani mwao na yeye atawafanyia hesabu pasi na pazia wala mkalimani.
18 – Inatkiwa kuamini Mizani siku ya Qiyaamah ambapo kheri na shari vitapimwa. [Mizani ina] viganja viwili na ulimi.
19 – Inatakiwa kuamini adhabu ya kaburi, pamoja na Munkar na Nakiyr.
20 – Inatakiwa kuamini hodhi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila Mtume ana hodhi isipokuwa tu Swaalih (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hodhi yake ni chuchu ya ngamia wake.
21 – Inatakiwa kuamini uombezi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watenda madhambi na waliokosea siku ya Qiyaamah na katika Njia. Atawatoa kutoka kwenye kina cha Moto. Hakuna Mtume isipokuwa ana uombezi na kadhalika wakweli, mashahidi na waja wema. Baada ya hapo Allaah ataonyesha fadhilah nyingi kwa yule anayemtaka na baada ya kuwa wameunguzwa na wamekuwa makaa, watatoka Motoni.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 72-73
- Imechapishwa: 16/12/2024
17 – Inatakiwa kuamini Kuonekana siku ya Qiyaamah. Watamuona Allaah (´Azza wa Jall) kwa macho yaliyo vichwani mwao na yeye atawafanyia hesabu pasi na pazia wala mkalimani.
18 – Inatkiwa kuamini Mizani siku ya Qiyaamah ambapo kheri na shari vitapimwa. [Mizani ina] viganja viwili na ulimi.
19 – Inatakiwa kuamini adhabu ya kaburi, pamoja na Munkar na Nakiyr.
20 – Inatakiwa kuamini hodhi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila Mtume ana hodhi isipokuwa tu Swaalih (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hodhi yake ni chuchu ya ngamia wake.
21 – Inatakiwa kuamini uombezi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watenda madhambi na waliokosea siku ya Qiyaamah na katika Njia. Atawatoa kutoka kwenye kina cha Moto. Hakuna Mtume isipokuwa ana uombezi na kadhalika wakweli, mashahidi na waja wema. Baada ya hapo Allaah ataonyesha fadhilah nyingi kwa yule anayemtaka na baada ya kuwa wameunguzwa na wamekuwa makaa, watatoka Motoni.
Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 72-73
Imechapishwa: 16/12/2024
https://firqatunnajia.com/04-watamuona-allaah-kwa-macho-yao/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)